Tuesday, August 22, 2023

Je WAJUA.. ?? KWANN KILA LENGO LAKO HALITIMII

 

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓

💦JE WAJUA...???💦

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓


🗣️Nakupa Siri Moja Muhimu Sana Kwenye Safari Yako Ya Utafutaji Yaah Hii Siri Endapo Utaifanyia Kazi Basi Asilimia Za Kufanikisha Mambo Yako Ni 💯 Hii Siri Haina Mbambamba Kabisa...


🧑‍✈️🧑‍✈️Ukitazama Picha Utaona Vijana Wa Jeshi La Kujenga Taifa(JKT) Unaweza Ukawa Unajiuliza Hii Picha Inahusiano Gani Na Mada Ya Leo Basi Kaa Kwa Kutulia Ndani Ya Muda Mfupi Ujao Utanielewa Kwanini Nimeiweka Hiyo Picha...


🧑‍✈️🧑‍✈️Natumaini Uwenda Wewe Unayesoma Huu Ujumbe Muda Huu Ushawahi Kupitia JKT Labda Ulienda Kama Kwamujibu Yaani Wale Waliomaliza Form Six Au Ulienda Kama Wakujitolea Ikiwa Na Maana Ni Wale Waliopitia Mchakato Wa Usahili Mikoani Hadi Kupata Hiyo Nafasi Au Ulishawahi Kusikia Story Za JKT Na Haujawahi Kwenda Bhasi Leo Tunazungumza Na Watu Wote Naamini Tutaelewana Tu...


🧑‍✈️🧑‍✈️Katika Sehemu Ambayo Wakiweka Malengo Yao Bhasi Lazima Yatimie Kwa Namna Yoyote Ile Ni JKT Yaani Hawa Jamaa Wako Seriously Sana Hawanaga Kubembeleza Mtu Uwe Unataka Au Hautaki Uwe Umechoka Au Unauvivu Utafanya Kazi Tu Kama Hautaki Ni Bora Urudi Kwenu Ila Sio Kukwamisha Kazi Zao...


🧑‍✈️🧑‍✈️Mtu Yoyote Aliyeenda JKT Atakama Alikua Hajui Kufanya Kazi Yaani Umetoka Kwenu Mboga 7️⃣ Ila Ukishatua JKT Utanyooka Tu Kazi Zote Utajua Sio Kulima Sio Kusafisha Mashamba Sio Kuhudumia Bustani N.K...


✍️✍️Sasa Siri Ambayo Leo Nitakujuza Ni Kwanini Wao Wakiweka Malengo Yao Lazima Yatimie Ila Wewe Ukiweka Malengo Yako Kutimia Huwa Ni Ngumu...


✍️✍️Nitakutajia Mbinu Wanazozitumia Na Endapo Mbinu Hizi Ukizitumia Katika Harakati Zako Za Utafutaji Mabadiliko Lazima Utayaona Kwa Kiasi Kikubwa Sana...


1️⃣ WANAFANYA VITU VYAO KWA MALENGO...


🧑‍✈️🧑‍✈️Siri Kubwa Wanayoitumia Watu Wa JKT Kutimiza Miradi Yao Haijalishi Ni Mikubwa Kiasi Gani Huwa Wanafanya Vitu Vyao Kwa Malengo (Target 🎯) Yaani Ukishatua JKT Lazima Kabla Ya Kuanza Kazi Mnajua Kabisa Lengo La Kazi Yenu Ni Lipi...??? Kama Ni Kusafisha Shamba Au Kulima Au Kuandaa Bustani Yaani Utajua Kwanza Kazi Yenu Inaishia Wapi Ili Kila Mmoja Ajue Yupo Pale Kwaajili Ya Kazi Gani Kwahiyo Katika Safari Yako Ya Upambanaji Hakikisha Unakua Na Malengo Na Unajua Unapambania Kitu Gani Hii Itakupa Mabadiliko Ni Tofauti Na Kuishi Bila Lengo Yaani We Upo Upo Tu...


2️⃣WANAUSIMAMIZI WA KINA KATIKA KAZI ZAO...


🧑‍✈️🧑‍✈️Bhana Bhana Ukiwa JKT Usitegemee Ipo Siku Utadanganya Sijui Unaumwa Au Sijui Utatoroka Kazi Zao 😂😂 Kule Kuna Usimamizi Asilimia 💯 Yaani Mtakua Watu Wengi Ila Kila Mmoja Lazima Awepo Sehemu Anayotakiwa Kwenye Hili Ata Mkiwa Watu Elfu 2️⃣ Sijui Elfu 3️⃣ Hauwezi Kutoroka(Kudoji) Kutokana Na Usimamizi Wao Kuwa Mkubwa Bhasi Yale Wanayoyapanga Huwa Yanatimia Kwahiyo Kama Na Wewe Unataka Kufanikiwa Hakikisha Unasimamia Vitu Vyako Kwa Kina Acha Uvivu Hakikisha Pale Unapotakiwa Kuwepo Uwepo Acha Kusimamia Miradi Yako Kwa Simu 📱 Uvivu Wako Ndio Unasababisha Vitu Vingi Kutokwenda Sawa...


3️⃣ UTAFANYA KAZI KATIKA HALI YOYOTE ILE IWE JUA IWE MVUA...


🧑‍✈️🧑‍✈️Kuna Ile Kawaida Ya Kudeka Yaani Ukiwa Unapambana Peke Yako Unajiamulia Tu Leo Sifanyi Kazi Sijui Leo Nimechoka Au Sijui Nitafanya Baadae Au Sio Lazima Kumaliza Kwasasa Yaani Unajipa Excuse Ambazo Muda Mwingine Hazina Maana Bhasi Tu Kwakua Wewe Ndio Boss Sasa Maisha Ya JKT Hayana Hiyo Wao Wakiwa Na Lengo Lao Haijalishi Umechoka Sijui Haujisikii Kufanya Kazi Sijui Mwili Unahisi Hauko Sawa Wao Iwe Jua Iwe Mvua Utafanya Kazi Ili Lengo Litimie Hakuna Kubembelezana Yaani Kwenye Hili Kama Hauamini We Nenda Utakuja Kutoa Ushuhuda Kwahiyo Ndio Maana Huwa Wanafanikiwa Na Wewe Unatakiwa Kwenye Harakati Zako Acha Kujipa Visingizio Hakikisha Unapambana Bila Kuchoka...


4️⃣ WANAZINGATIA MUDA KULIKO KAWAIDA...


🧑‍✈️🧑‍✈️Hakuna Sehemu Ambayo Wanazingatia Muda Kama Jeshini Yaani JKT Muda Wote Unazingatiwa Utakua Sehemu Husika Kulingana Na Ratiba Yao Kama Ni Muda Wa Shamba Bhasi Watu Wote Watakuwepo Shamba Kama Ni Muda Wa Chakula Bhasi Watu Wote Watakuwepo Kwenye Chakula Kwahiyo Kuishi Kwa Kuzingatia Na Kuthamini Muda Ni Njia Moja Wapo Ya Kukufanya Ufanikishe Mambo Yako...


5️⃣MWISHO KABISA WANAISHI KWA RATIBA (TIME TABLE)...


🧑‍✈️🧑‍✈️Maisha Ya JKT Yamefungamana Na Ratiba Muda Wote Yaani Ukiwa Kule Tambua Muda Fulani Natakiwa Kuwa Sehemu Fulani Tunaweza Sema Ni Ratiba Ya Siku Nzima Kuanzia Muda Wa Kuamka Hadi Muda Wa Kulala Kwahiyo Mafanikio Siku Zote Yanatengenezwa Na Siku Yako Umeitumia Vipi Haijalishi Unamalengo Ya Miaka 5️⃣ Kama Siku Inapitia Bila Nidhamu Hakuna Hatua Utakayopiga Mafanikio Yaanza Na Siku Yako Unavyoitumia Kwahiyo Kama Unataka Kufanikiwa Hakikisha Siku Yako Unaitumia Na Kuifanyia Kazi Ili Ufikie Malengo Yako Ila Kama Unaishi Kama Kunguru Wewe Ni Kuamka Kuzurura Na Baadae Kurudi Kwenye Kiota Sahau Kufikia Malengo Yako... 


✍️✍️Mtafute Mtu Aliyepitia JKT Muulize Kuhusu Haya Yote Niliyoyaeleza Atakuambia Yanaukweli 💯 Ila Sasa Watu Wakishapitia Maisha Ya JKT Wanashindwa Kuchukua Yale Mafunzo Waliyoyapata Na Kuyafanyia Kazi Katika Harakati Zako Kwasababu Wanatoka Na Hisia Kuwa Walikua Kwenye Mateso Na Sio Kujifunza Maisha...


✍️✍️Nakushauri Hakuna Mafanikio Mepesi Ukiona Mtu Kafanikiwa Kwa Jambo Lolote Jua Kuna Mpito Usio Wa Kawaida Kaupitia Kwahiyo Tukubali Kuumia Kwaajili Kesho Yetu Iwe Bora Zaidi...


🙏 Hongera Sana Naamini Sasa Umeshajua 🙏

Monday, August 21, 2023

JE WAJUA KUANZA CHINI NI BORA KULIKO UNAVYO DHANI


 🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓

💦JE WAJUA...???💦

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓


🗣️Kama Umemaliza Chuo Upo Tu Mtaani Na Haujui Ufanye Nini Naomba Nikushauri Kitu Kama Hautojali Ila Ujumbe Huu Ni Kwa Watu Wote Ata Wewe Unakufaha Pia...


🧑‍🏫🧑‍🏫Kabla Ya Kuendelea Na Ushauri Wetu Naomba Chukua Mda Huu Kushare Ili Ujumbe Huu Uwafikie Watu Wengi Na Kama Haujajiunga Na Page Yetu Hakikisha Unabonyeza Hapa 👉https://maarifa-media.blogspot.com

Kisha Jiunge Nasi Karibu Sana...


✍️✍️Najua Baada Ya Kumaliza Chuo Na Kujikuta Upo Tu Home Unatamani Kuanza Biashara Yoyote Ilimradi Uweze Kutimiza Malengo Yako Ni Jambo Zuri Hongera Kwa Hilo👏👏👏...


✍️✍️Najua Kuna Vitu Vinakukwamisha Kuchukua Maamuzi Ya Kuanza Licha Ya Hofu Ya Kuthubutu Ila Hivi Vitu 3️⃣ Endapo Utaishi Navyo Vitakuchelewesha Sana Kuchukua Maamuzi Sahihi Sasa Tuchambue Hivyo Vitu Hili Uweze Kuepukana Navyo Mapema Kabla Ya Kuendelea Kukutafuna...👇👇👇


1️⃣Hauko Tayari Kuanza Chini...

✍️Najua Ulikua Na Ndoto Kubwa Na Shule Ilikua Inakuandaa Kuwa Boss Sasa Baada Ya Kumaliza Bado Unajiona Ni Mtu Wa Hadhi Kubwa Hautaki Kufanya Shughuli Yoyote Huku Ukijifariji Kusubiri Ajira Na Mda Unazidi Kukutupa Mkono...


✍️Najua Wengine Mna Mtaji Wa Kuanza Biashara Ila Unaona Aibu Kuanza Chini Yaani Bado Unamawazo Kama Utaanza Biashara Bhasi Uanze Kwa Ukubwa My Friend Unajichelewesha...


✍️Amka Amka Amka Chukua Maamuzi Maisha Ni Yako Hizo Aibu Hazikusaidii Chochote Toka Kwenye Huo Usingizi Umri Unazidi Kwenda Sitaki Uje Kujilaumu Mbele Ya Safari Ndio Maana Nimeandika Hii Somo Kwaajili Yako Kama Unaona Mazingira Ya Hapo Ulipo Wengi Wanakujua Kwahiyo Hautakua Huru Hamia Ata Mkoa Mwingine Nenda Kapambane Na Sio Kuendelea Kutumia Gharama Kubwa Kuwaaminisha Watu Umefanikiwa Kumbe Bado Unajitafuta...


2️⃣Acha Kujifanya Mjuaji Kubali Kujifunza Ata Kwa Uliowazidi Elimu...

✍️Elimu Yako Isikufanye Uwe Kipofu Kwa Kudharau Wengine Hapo Elimu Yako Itakua Haina Manufaa Na Wewe Tambua Maisha Ya Mtaani Ni Tofauti Na Elimu Ya Darasani Ndio Maana Watu Wanasema Kuna Elimu Ya Kitaa...


✍️Tafuta Maarifa Ukiwa Mtaani Jifunze Kwa Watu Fanya Udadisi Kwa Kutumia Uwezo Ulionao Kisha Tafuta Namna Ya Kutatua Matatizo Ya Mtaani Kupitia Suluhisho Lako Utajikuta Unapata Pesa Kuliko Kuendelea Kujifungia Ndani Na Kuona Watu Wa Mtaani Sio Hadhi Yako...


✍️Zingatia Hili Elimu Yako Itakupa Uwezo Mkubwa Wa Kutambua Vitu Kwa Haraka Ila Thamini Watu Kwasababu Kupitia Watu Ndio Utapata Kitu...


3️⃣Acha Kuishi Kwa Mashindano...

✍️Tunajua Umemaliza Chuo Na Pia Jamii Inajua Ajira Ni Ngumu Kipindi Hiki Bhasi Acha Kuishi Maisha Fake Yaani Unapambana Kuonyesha Watu Kuwa Umefanikiwa Kumbe Upo Kwenye Kujitafuta...


✍️Tafuta Connection Kwa Watu Waliokuzunguka Ishi Na Watu Vizuri Weka Uhalisia Wa Maisha Yako Itakupa Uwepesi Wa Kupata Michongo Ya Kufanya...


✍️Kama Umemaliza Chuo Na Unataka Kushindana Na Watu Ili Uonekane Sio Mnyonge Ndugu Yangu Maisha Ya Maigizo Yatakumalizia Pesa Tu Na Hutachelewa Kufikia Malengo Yako...


🙇🙇Tunakupenda Na Tunatamani Ufanikiwe Ndio Maana Tumechukua Mda Huu Kukushauri Chukua Unayoona Yatakufaa Ambayo Unaona Hayana Umuhimu Tuachie...🙇🙇


💞 Mwenyezi Mungu Akufungulie Riziki Kwenye Ugumu Akuwekee Wepesi Na Kwenye Giza Akuwekee Nuru Ya Ku🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓

💦JE WAJUA...???💦

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓


🗣️Kama Umemaliza Chuo Upo Tu Mtaani Na Haujui Ufanye Nini Naomba Nikushauri Kitu Kama Hautojali Ila Ujumbe Huu Ni Kwa Watu Wote Ata Wewe Unakufaha Pia...


🧑‍🏫🧑‍🏫Kabla Ya Kuendelea Na Ushauri Wetu Naomba Chukua Mda Huu Kushare Ili Ujumbe Huu Uwafikie Watu Wengi Na Kama Haujajiunga Na Page Yetu Hakikisha Unabonyeza Hapa 👉https://maarifa-media.blogspot.com

Kisha Jiunge Nasi Karibu Sana...


✍️✍️Najua Baada Ya Kumaliza Chuo Na Kujikuta Upo Tu Home Unatamani Kuanza Biashara Yoyote Ilimradi Uweze Kutimiza Malengo Yako Ni Jambo Zuri Hongera Kwa Hilo👏👏👏...


✍️✍️Najua Kuna Vitu Vinakukwamisha Kuchukua Maamuzi Ya Kuanza Licha Ya Hofu Ya Kuthubutu Ila Hivi Vitu 3️⃣ Endapo Utaishi Navyo Vitakuchelewesha Sana Kuchukua Maamuzi Sahihi Sasa Tuchambue Hivyo Vitu Hili Uweze Kuepukana Navyo Mapema Kabla Ya Kuendelea Kukutafuna...👇👇👇


1️⃣Hauko Tayari Kuanza Chini...

✍️Najua Ulikua Na Ndoto Kubwa Na Shule Ilikua Inakuandaa Kuwa Boss Sasa Baada Ya Kumaliza Bado Unajiona Ni Mtu Wa Hadhi Kubwa Hautaki Kufanya Shughuli Yoyote Huku Ukijifariji Kusubiri Ajira Na Mda Unazidi Kukutupa Mkono...


✍️Najua Wengine Mna Mtaji Wa Kuanza Biashara Ila Unaona Aibu Kuanza Chini Yaani Bado Unamawazo Kama Utaanza Biashara Bhasi Uanze Kwa Ukubwa My Friend Unajichelewesha...


✍️Amka Amka Amka Chukua Maamuzi Maisha Ni Yako Hizo Aibu Hazikusaidii Chochote Toka Kwenye Huo Usingizi Umri Unazidi Kwenda Sitaki Uje Kujilaumu Mbele Ya Safari Ndio Maana Nimeandika Hii Somo Kwaajili Yako Kama Unaona Mazingira Ya Hapo Ulipo Wengi Wanakujua Kwahiyo Hautakua Huru Hamia Ata Mkoa Mwingine Nenda Kapambane Na Sio Kuendelea Kutumia Gharama Kubwa Kuwaaminisha Watu Umefanikiwa Kumbe Bado Unajitafuta...


2️⃣Acha Kujifanya Mjuaji Kubali Kujifunza Ata Kwa Uliowazidi Elimu...

✍️Elimu Yako Isikufanye Uwe Kipofu Kwa Kudharau Wengine Hapo Elimu Yako Itakua Haina Manufaa Na Wewe Tambua Maisha Ya Mtaani Ni Tofauti Na Elimu Ya Darasani Ndio Maana Watu Wanasema Kuna Elimu Ya Kitaa...


✍️Tafuta Maarifa Ukiwa Mtaani Jifunze Kwa Watu Fanya Udadisi Kwa Kutumia Uwezo Ulionao Kisha Tafuta Namna Ya Kutatua Matatizo Ya Mtaani Kupitia Suluhisho Lako Utajikuta Unapata Pesa Kuliko Kuendelea Kujifungia Ndani Na Kuona Watu Wa Mtaani Sio Hadhi Yako...


✍️Zingatia Hili Elimu Yako Itakupa Uwezo Mkubwa Wa Kutambua Vitu Kwa Haraka Ila Thamini Watu Kwasababu Kupitia Watu Ndio Utapata Kitu...


3️⃣Acha Kuishi Kwa Mashindano...

✍️Tunajua Umemaliza Chuo Na Pia Jamii Inajua Ajira Ni Ngumu Kipindi Hiki Bhasi Acha Kuishi Maisha Fake Yaani Unapambana Kuonyesha Watu Kuwa Umefanikiwa Kumbe Upo Kwenye Kujitafuta...


✍️Tafuta Connection Kwa Watu Waliokuzunguka Ishi Na Watu Vizuri Weka Uhalisia Wa Maisha Yako Itakupa Uwepesi Wa Kupata Michongo Ya Kufanya...


✍️Kama Umemaliza Chuo Na Unataka Kushindana Na Watu Ili Uonekane Sio Mnyonge Ndugu Yangu Maisha Ya Maigizo Yatakumalizia Pesa Tu Na Hutachelewa Kufikia Malengo Yako...


🙇🙇Tunakupenda Na Tunatamani Ufanikiwe Ndio Maana Tumechukua Mda Huu Kukushauri Chukua Unayoona Yatakufaa Ambayo Unaona Hayana Umuhimu Tuachie...🙇🙇


💞 Mwenyezi Mungu Akufungulie Riziki Kwenye Ugumu Akuwekee Wepesi Na Kwenye Giza Akuwekee Nuru Ya Kuona....💞


🙏Kila La Kheri Ndugu 🙏ona....💞


🙏Kila La Kheri Ndugu 🙏

Saturday, July 22, 2023

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI

 

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUWI 

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini

5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r

elated cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi

18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita


BLEND KAMA UNAVYO TENGENEZA JUICE YA KAWAIDA KISHA KUNYWA GLASS MOJA KWA SIKU. 


AU UNAWEZA KUJENGA MAZOEA YA KUTAFUNA VIPANDE KADHAA KILA SIKU ASUBUHI KABLA HUJALA KITU 


AFYA KWANZA HERBAL CLINIC TUNAJALI AFYA YAKO

Sunday, July 9, 2023

PICHA INAANZA STAR KAFA... STORY KWA UFUPI

          ........STORY KWA UFUPI 

STORY KWA UFUPI


Kundi la maprofesa waliitwa na kuketi kwenye ndege kwa ajili ya mkutano. 

Milango ilipofungwa na ndege ikakaribia kupaa, maprofesa wote walifahamishwa kuwa ndege hii imetengenezwa na wanafunzi wao. Maprofesa walivyosikia hivyo wakaamka kwa ajili ya kutoka nje wote wakakimbilia kwenye milango ya ndege wakijaribu kutoroka isipokuwa profesa mmoja alibaki ameketi kwa ujasiri na utulivu mwingi. Kuna mtu alimuuliza kwanini hujaribu kutoka kwenye ndege. Profesa akamjibu kwa kujiamini, "ni wanafunzi wetu." 

Akamuuliza tena "una uhakika kwamba uliwafundisha vizuri?" 


Profesa akajibu kwa sauti ya chini "Nina uhakika hii ndege haitapaa". 😃😃


Endelea sana kuja kwenye hii Blog post kuna mambo mazuri kila siku 

Thursday, June 29, 2023

MAITI INAYO TEMBEA

 Maiti inayo tembea sehemu ya kwanza 


Maiti inayotembea


Sehemu Ya 1


 jama mimi sijafa fungueni jeneza nirudi kwenye kiwiliwili changu... hakuna mtu aliye msikiliza peto wala kumjali.. jeneza lilitolewa nje na kuwekwa juu ya meza tayari kwa kuuaga mwili wa marehem... peto alimfuta mwanae chales na kumwambia ebu fungua jeneza mwanangu... nitakupa kila kitu unachokitaka.... chales hakumjali baba yake alibaki kimya""


jeneza lilifunguliwa upande wa kichwani... na watu wakajipanga kwenye mstari mmoja kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu peto... peto alipo ona jeneza limefunguliwa alifurahi sana alitimua mbio kuelekea pale jeneza lilipokuwepo ili aungane na kiwiwili chake.... alipofika alijaribu kuingia lakini alistahajabu sana.. kashindwa kuungana na kiwiliwili chake... kisha akasema ""jamani kiwiliwili changu mimi ni nafsi yako.....nihurumie""" mmh!! inamaana nazikwa huku najiona hivi hivi.... yani hata kiwiliwili changu kinanikana mimi nafsi yake.. 

kumbe ili nafsi ya peto iungane na kiwiliwili ni lazima kiwiliwili kirudishwe pale kitandani kilipokuwa...


peto alianza kulia kwa uchungu....baada ya watu waliohudhulia msiba wa peto walimaliza kuaga mwili wa marehem peto.... na kujiandaa kuelekea makaburini kwa ajili ya kuuzika.. peto alizidi kuchanganyikiwa.. baada ya kuona jeneza lake likibebwa kupelekwa ndani ya gari.


Peto alianza kuangua kilio... alipiga mayowe ya kuomba msaada bila mafanikio yoyote... alimshi dereva... ili ahairishe kuendesha gari kuelekea makaburini.. dereva hakumjali peto... alibaki kimya huku akionesha wazi kutomsikia peto anaongea nini"" kisha dereva akazipiga hatua kuelekea upande mwingine... jamani mbona binadamu hamna huruma... alijisemea peto huku akilia kwa uchungu... peto hakukata tamaa aliendelea kuwasihi watu waliohudhuria msiba wale wasizike kiwilwili chake... aliamini huenda wakamsikia... peto aliamua kuchukuwa mawe mawili na kuyaweka chini ya matari ya gari ili lisiondoke.... kwa mbali alimuona chales akiingia upande wa ndani ya nyumba.... peto alitimua mbio kuelekea mule ndani alimoingia chales...peto alipofika alimwambia chales mwanangu tazama mimi baba yako ninavyoangaika!!!! nionee huruma mwanangu... ebu fikiria kama watazika kiwiliwili changu itakuwaje? ni nani atakaye kutunza zaidi ya mimi baba yako....ebu jaribu kuwaambia watu warudishe kiwiliwili changu kitandani kwangu hienda kikakubali kuungana na nafsi yangu" peto aliyasema maneno hayo huku akilia kwa uchumgu mkubwa.... wakati huo chales alikuwa kaketi chumbani kwake huku kashika tama akilia huku akimkumbuka marehemu baba yake.....hakika nilikupenda sana baba yangu lakini mungu kakupenda zaidi...alijisemea moyoni chales""huku akilia kwa uchungu... jamani mwanangu unalia nini mimi sijafa... alisema peto"" chales alionekana kuwa kimya bila kujibu chochote...


kisha akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kuelekea upande wa nje... Peto alianza kuingiwa matumaini huwenda sasahivi mwanae kamsikia alichokuwa akimwambia ndio maana anatoka nje... asante mwangu kawaambie" peto alisema hivyo.. kisha akazipiga hatua kumfata chales kule upande wa nje.


**************


peto alipofika nje alistahajabu sana..kumuona chales akipitiliza na kwenda kuketi.... agh inamaana hakusikia yale yote niliyokuwa nikimwambia!!!! peto alijisemea moyoni""sasa hapo peto alianza kumkumbuka mungu aliamini mungu anao uwezo kuliko binadamu.......peto. alipiga magoti na kuanza kumuomba mungu huenda wakahairisha kizika kiwiliwili chake.... peto aliomba huku akilia kwa uchungu.. uso na macho yake yalionesha wazi kujutia..masanja umeniponza mimi laiti ningejua nisingekubaliana na wewe kunipeleka kujiunga na chama cha wachawi... tazama sasa hata nyinyi wachawi wenzangu mmeshindwa kunisaidia mimi mwenzenu!!!!! alisema peto huku akilia na kugalagala chini.....alipo ona hakuna msaada wowote aliamua kunyanyuka pale chini... aliona wakina mama wakilia kwa uchungu...hata yule jirani aliyetaka kuuliwa kichawi na mke wa peto naye alilia kwa uchungu mkubwa... pete alizidi kuchanganyikiwa alipo ona watu wengine walilia mpaka kuzimia.... peto aliweka mikono kichwani huku akiwatazama watu wakilia.... hivi hawa akinamama nahisi akili zao sio nzuri uani wanamlilia mtu ambaye hajafa!!!! alijisemea moyoni peto,,, kisha akapaza sauti jamani tusikilizane mimi sijafa embu acheni mchezo na kiwiliwili changu... watu hawakuonesha kumjali peto.... kisha akaona watu wakiingia ndani ya magari ili waelekee makaburini..... peto alizidi kuchanganyikiwa..watu wote waliingia ndani ya magari na wengine wakitembea kwa miguu kuelekea makaburini... alipotazama huku na kule aliona watu wanazidi kupungua.... aliamua kuzipiga hatua za haraka akaingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili chake.... na safari ya kuelekea makaburini ikaanza


Alionekana derva akiingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili cha peto.. dereva alipoliwasha gari peto alichanganyikiwa... safari ikaanza"" makaburi hayakuwa mbali sana iliwachukuwa dakika 45 kufika makaburini... walipofika.. Peto alikuwa wa kwanza kushuka... kwa mbali aliona mafundi wajenzi wakiwa wanachanganya zege.... peto alizidi kuchanganyikiwa aliamini bila shaka mafundi wale walikuwa wakiandaa zege kwa ajili ya kaburi lake... alitimua mbio mpaka pale walipokuwepo mafundi.. alipofika alichungulia ndani ya shimo... jamani mbona hamna huruma inamaana ndio mnazika humu kiwiliwili changu... kisha akawatazama mafundi wale alimuona fundi mmoja aliyekuwa akimfahamu alimsogelea na kumsihi wasizike kiwiliwili chake""'" fundi eee kwani haunikumbuki??? mimi peto na sijafa....aliongea peto huku uso wake ukionekana kuwa na huzuni kubwa... fundi yule hakumjibu peto aliendelea kuchanganya simenti na mchanga vikiambatana na kokoto" huku akipiga stori na mafundi mwenzake.....yule fundi mwingine alisikika akisema ongeza simenti zege iwe kali...peto aliposikia hivyo alitamani amnyang'anye koleo fundi. alijaribu kufanya hivyo lakini alishindwa..... alipotazama upande wa kushoto aliona watu wakiwa wamebeba jeneza wakija huo upande aliokuwepo peto... peto alianza kulia.. alibaki akiwatazama watu wale... jamani hivi kweli hawanisikii au wanataka kunikomoa tu!!!! eti fundi hamnisikii??? alisema peto"" mafundi wale hawakumjibu kitu waliendelea kufanya kazi yao. nakuonekana kutomjali.. punde jeneza lililetwa likawekwa kando ya kaburi... peto aliweka mikono yake kichwani.... na kuangua kilio kwa kupiga mayowe.... lakini haikusaidia kisha alionekana mchungaji akija upande wa kaburi ili auwombee mwili wa marehem peto....... watu wote walifumba macho kisha mchumgaji akaendelea na maombi.. peto aliona huo ndio muda mzuri wa kufingua jeneza aingie kwenye kiwiwili chake. alipojaribu kulifungua jeneza alishindwa..


****************


punde mchungaji alimali maombi.... peto aliona watu wanachukua kamba na kuziweka katijeneza kisha wakaanza kulishutaratibu kuliingiza nadani ya kaburi... aisee peto aliangua kilio...alijaribu kuwazuia watu wale wasiliingize jeneza kaburini lakini alishindwa.... punde walimaliza kuliingiza jeneza kisha mchungaji akasema mtoto wa marehemu ataanza kuweka mchanga kwenye kaburi la baba yake huku akifatiwa na ndugu na jamaa wa karibu na peto... chales alichota mchanga na kutupa ndani ya kabiri.. huku akilia kwa uchungu.. baba yangu inamaana sitokuona tena?? chales alisema huku analia""" peto alipaza sauti mwanangu mimi sijafa yani hata wewe unakubali kubali kunizika mzimamzima hivi najiona"""" chales aliendele kutupa mchanga ndani ya kaburi na kuondoka.. walifuta ndugu na jamaa pamoja na marafiki wa peto.... walipo maliza""" watu walianza kuchukua makoleo na kuanza kufukia kaburi la peto... mara ghafla....ilisikika sauti ya mngurumo mkubwa ikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu... watu walianza kuogopa hata peto iwoga ilianza kumuingia.... watu waliokuwa wakilifukia kaburi la peto waliacha kufukia... huku wakistahajabu upepo huo unaovuma kwa kasi isiyo ya kawaida... mara ghafla peto aliona watu wakija ule upande wa kaburi alipoangalia kwa umakini aligundua ni wale wachawi wenzake wakiongozwa na Magembe ambaye ni mkuu wa wachawi... walipokaribia mara ghafla jeneza la peto lilianza kutoka kunako ndani ya kabiri likija upande wajuu na kujiweka kando ya kaburi.... watu walitimua mbio hakibaki hata mtu mmoja""""hata yule mchungaji alitimua mbio kutokana imani yake kuwa ndogo... peto alipo ona mpaka mchungaji katimua mbio ilibidi na yeye atimue mbio peto alikimbia utadhani alishawahi kushiriki mashindano ya mbio za mita mia....


magembe na wachawi wenzake walilifiata kaburi kisha wakasimama karibu na jeneza la peto... mara ghafla....


peto alikimbia mara ghafla akasita kuendelea kukimbia.. akasimama... dah!! hivi mimi ni mjinga kiasi gani? huenda wamekuja kunisaidia... alipogeuka atazame ule upande lilipokuwepo kaburi lake... aliona Magembe...Masanja pamoja na wachawi wengine watatu wamelizunguka jeneza lake..... ghafla wakatoweka pamoja na jeneza....peto alichanganyikiwa akapaza sauti huku anakimbia kurudi kule lilipokuwepo jeneza lake... jamani eee mbona mmenisahau nipo huku"" Magembe unapeleka wapi kiwiliwili changu??peto alisema maneno hayo huku anakimbia kwa kasi kama kafungwa mota miguuni... alikata tamaa na kuamua kuondoka haraka aende nyumbani kwa magembe. ...akiwa njiani anazipiga hatua aliona mtu anasukuma mkokoteni huku kabeba mzigo..alipotazama vizuri aligundua ni mkokoteni wake .. alimfata mtu huyo... kisha akamwambia.... mbona unatumia kitendea kazi changu bila ruhusa yangu??? mtu yule alibaki kimya hakumjibu peto....peto alikasirika sana.. akaanza kukunja mikono ya shati yake ili aanzishe ugomvi... ghafla akakumbuka kiwiliwili chake... akaanza kutimua mbio kielekea kule nyumbani kwa magembe... alipofika hakumkuta magembe.... hivi hawa watu mbona wanafanya mchezo na kiwiliwili changu!!!? peto alijisemea moyoni"""" punde magembe ambaye ndiye mkuu wa wachawi alikuja nyumbani kwake.....huku akiwa amemuacha masanja na wale wachawi wengine wapeleke kiwiliwili cha peto nyumbani kwa peto pale juu ya kitanda ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake"""magembe alikuwa na iwezo wa kumuona peto... kisha akamwambia ndani ya masaa matatu.. inatakiwa uwe umeshaungana na kiwiliwili chako.... sharti... itabidi utoe kafara la damu ya mtoto wako.... peto alichanganyikiwa baada ya kusikia masharti ya magembe..... peto aliamua kukubali..... kisha akajisemea moyoni.....nikiungana na kiwiliwili changu tu.....naacha uchawi na sitoweza kumtoa mtoto wangu kafara...."""""" magembe alimwambia peto waweza kwenda.... peto alianza kutimua mbio kuelekea nyumbani kwake..


*********


uleupande mwingine.. Masanja na wale wachawi wengine waliwasili nyumbani kwa peto... wakatokezea upande wa nyuma ya nyumba ya peto...kisha masanja akaingia kichawi ndani ya nyumba ya peto ili aangalie mazingira yamekaaje.... alipoingia kwenye chumba cha peto masanja alistahajabu kukuta chumba cha peto hakuna kitu ndani hata kitanda ambacho inatakiwa iwekwe maiti ya peto...ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake...kumbe chales alikifungua kitanda hicho na kukiweka stoo ili atandike mkeka mkubwa ipatikane nafasi ya kulala wageni waliosafiri kuja msibani......


wakati huohuo peto alikuwa njiani akitimua mbio kuja nyumbani kwake.. punde alifika.. alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake ili aungane na kiwiliwili chake.... alikutana uso kwa uso na masanja... masanja hakuwa na uwezo wa kumuona peto isipokuwa Magembe pekee. ..peto alistahajabu kuona hakuna kitanda wa kitu chochote....kisha akamuuliza masanja kiwiliwili changu kikowapi?? masanja hakujibu kitu.. alitoweka kichawi....wee rudi hapa nipeni kiwiliwili changu""alisema peto kwa sauti ya ukali"""


masanja alitokezea upande wa nyuma ya nyumba kule alipowaacha wachawi wenzake na kiwiliwili cha peto. .....na kusema hii kazi itakuwa ngumu sana kisha wakatoweka kichawi kuelekea kwa mkuu wa wachawi Magembe....huku wakiliacha hapo chini jeneza la peto...


*********


Peto alitoka mule chumbani na kuelea upande wa nje.. alimuona mwanae chales akamfata na kumwambia kitanda changu kikowapi??? chales alibaki kimya...peto alizidi kuchanganikiwa aliamua kurudi ndani na kutazama saa ya ukutani ilikiwa ni saa kumi na moja... lisaa limojs limshakwisha.....peto alianza kuingiwa na uwoga wa hali ya juu aliamua kutokea mlango wa nyuma... alistuka kuliona jeneza lake... akazipiga hatua za taratibu kulifiata jeneza lilipokuwa..... alipofikaara ghafla..


Aliona jeneza linafunguka peke yake bila kufunguliwa na mtu.... peto aliona kiwiliwili chake alipojaribu kurudi aungane na kiwiliwili chake alishindwa""" dah! yani hata wewe unanikataa mimi nafsi yako embu kuwa na huruma!!!! tazama yamebaki masaa mawili tu.... niliyopewa ili nirudi kwenye kiwiliwili changu""" alisema peto akikiambia kiwiliwili chake..... huku akionesha sura ya upole....na huzuni kubwa.. peto aliamua kutoka upande ule na kuelekea upande wa mbele ya nyumba...... alianza kupiga mayowe kwa sauti kubwa... jamani eee nimebakiza masaa mawili tu.....nyinyi ndio mtasababisha mimi nife!!!!! watu hawakumjali ndio kwanza waliendelea kunawa mikono na kula chakula....aisee inamaana nakufa hivihivi nikiona!!!!!? alijiuza kimoyoni kisha akakunja suruali akaanza kutimua mbio kurudi nyumbani kwa mkubwa wa wachawi ambae ni Magembe... peto alikimbia bila kugeuka nyuma"" alipofika alichanganyikiwa baada ya kutomkuta magembe.... Mbona mnaniangaisha hivi... haki naapa nikifanikiwa kurudi kwenye kiwiliwili changu.. naokona na kuanza kumtumikia Mungu""" Eee Mungu nisaidie tazama navyoteseka!!!!!!


Itaendelea







Utamu wa nyama za watu

Sehemu ya 1


🥩😋Utamu wa nyama za watu😋🥩


Sehemu ya 1


Nilikaa peke yangu chini ya mwembe mkubwa, watoto wengine ambao ni marafiki zangu walikuwa wakicheza uwanjani kando ya mwembe huo. Nilikaa kimya nawatazama tu na macho yangu mabaya ya Kichawi.


Nyuma ya mwembe kulikuwa na makaburi hayakuwa mengi. Hayakuwa mengi kwa sababu yalikuwa maalum kwa ajili ya kuwazika Mashehe na MAUSTADH wakubwa wa Kijiji chetu.

Kando kidogo ya hayo makaburi kulikuwa na msikiti, msikiti wa Kijiji chetu.


Watu walimaliza kuswali swala ya saa kumi na wakawa wanarudi majumbani kwao. Mimi bado nilikuwa nipo peke yangu nimekaa Kimya.


"Haujambo" Nilisikia sauti ya Mzee mmoja aliyevalia kanzu iliyochakaa. 


Niligeuka na kumtazama hakuwa peke yake bali walikuwa wawili na wote walikuwa wakitoka Msikitini kuswali.


"Sijambo" Niliwajibu 

"Mbona hutuamkii?" waliniuliza. 


Mimi sikuwajibu chochote nilikaa Kimya.

Yule Mzee mmoja akaninyooshea mkono na kunipa kitu.


Nilipotazama hakikuwa kitu bali lilikuwa Jini lilitongenezwa kichawi 

lilikuwa linatoa harufu mbaya km ya usaha.

Nikalipokea lile Jini na kulishika.


"Tunamtaka Mtoto wa Mwajuma anaeitwa Zuberi" waliniambia wanataka nimtupie Jini mtoto wa Mwajuma.


Sikuwajibu niligeukia pembeni kwa maana nilikuwa tayari nimekubali walichonituma.

Wale wazee Wawili wakaondoka.


Hapo Mimi nikanyanyuka na kuondoka zangu.

Nilienda hadi kwa mama Zuberi nikamkuta anamuogesha mtoto wake aitwaye Suma, mie nikasimama uwanjani kwao.


Wakati huo Zuberi alikuwa akicheza Gololi na mtoto wa jirani yao hapo hapo kwao.

Mwajuma aliponiona tu akasonya.


"Wenzako wanarithi kulima we unarithi uchawi, Mtoto mdogo lkn mwanga na utawatisha hao hao Mimi na Mume wangu tumeaga kwetu" 

Aliniambia Mwajuma 

Na ni kweli Mwajuma alijikinga vilivyo alikuwa hawezekani kirahisi na ndio maana wale wazee Wawili walishindwa kabisa kumuingia.


Akampeba Suma Mgongoni kisha akamwaga yale maji,

Wakati anayamwaga Yale maji nikamka maneno ya Kichawi kimoyo moyo 

Yale maji yakachelewa kuzama chini lkn Yeye hakuyaona lilikuwa Ni tendo la Kichawi Kisha Mimi nikasogea na kuliweka Jini ndani ya maji. 


Kwa UCHAWI na miujiza Sasa Lile jini likajitutumua km lipo Baharini, Ni mfano wa Kitu kisichoelezeka kiwepesi. Manyoya km ya mkia wa ng'ombe, halafu Ni Rangi ya njano ya usaha, km Mtoto asiyekamilika Akiwa tumboni.

Mimi nikaondoka zangu 

Sasa nikajua kwa vyovyote vile Zuberi atalivaa Lile Jini.


Nikaelekea kwenye Mti Mkubwa porini unaitwa MKATA KAULI

Nikakata Gome lake pamoja na mizizi yake iliyokuwa km kamba kamba, nikavishika vyema.

Nikatoka mbio kutoka hapo porini Hadi Makaburini nikazunguka pembe zote Nne wazoingilia watu wakienda kuzika

Na kila pembe Nikawa nauchota mchanga.

Sasa Giza likawa linaanza kuingia.

Nikaita mara Saba


"MWAJUMA X 7" Huku naumimina ule mchanga kwenye Gome la mti la mkata kauli.

Nilipomaliza hapo nikaufunga km Maiti Kupitia mizizi ya Mti wa mkata Kauli.

Licha ya kuwa na Giza lkn Sikuwa muoga.

Nikaenda Shambani huko Kuna migomba(Midizi) Nikautafuta mgomba Mkubwa Sana lakini Ulio inama.

Nikachukua jiti na kuchimba chini kwenye shina la mgomba, nikaipita mizizi na kuwa na shimo lefu.

Hapo Sasa Nikawa na Vitu VINNE NILIVYOVITAKA


1- MKATA KAULI (NITAMKATA KAULI MWAJUMA ASISEME CHOCHOTE KUHUSU MIMI MAANA ALINIONA"


2- MIZIZI YA MKATA KAULI ( NIMEMFUNGA NA MIZIZI KM KAMBA ITAKAYOMFANYA H

ASHINDWE KUTEMBEA, KUTOKA KWENDA KUTAFUTA DAWA WALA KINGA KWA MGANGA)


3- MCHANGA WA MAKABURINI (AWE WA KUSEMA TU BORA MWANANGU AFE AZIKWE KULIKO KUTESEKA YANI NI SAWA NIMEMKATISHA TAMAA AONE KUMZIKA MTOTO NDIO SULULISHO) Hii pia huwakuta watu Wengi MITAANI unaona Bora Ndugu yako afe kuliko KUTESEKA kumbe sio Akili yako.


4- MGOMBA ULIO INAMA (YOTE KWA YOTE NAMUINAMISHA NA ANAKUWA CHINI YANGU NA SIO CHINI YA AMRI ZA MUNGU HAPO UCHAWI WANGU UNATEMBEA KWENYE MWILI NA NAFSI YAKO.


Hapo nikafukia (kukuzika) Mchanga na Lile Gome la mti wa mkata kauli kwenye Shimo nililochimba.


Ndugu Msomaji ukisikia Kuroga / kurogwa ndio kwa Namna hiyo.


Baada ya kufanya hivyo nikarudi Nyumbani kwetu. Hakukuwa na Mtu yeyote, sio baba Wala mama hata Kaka zangu.

Watu wote walikuwa Msibani, Msiba wa mtoto wa MCHUNGAJI aliyekufa kwenye mazingira ya kutatanisha

Nilipoingia ndani chumbani kwangu juu ya kitanda nikakuta kifurushi cha pesa, sio pesa ndogo zilikuwa pesa nyingi.


Sikushangaa nilijua wale wazee Wawili wa Kichawi wamekuja kunipa Pesa km malipo. Na ukiwaangalia wao Ni masikini wa kutupwa lkn walikuwa na Uwezo wa kukulipa pesa yoyote hata yawe mabilioni endapo tu mtakapo kubaliana.


Siku za Mbele nitakuelezea WACHAWI WANAWEZAJE KUPATA PESA NYINGI NA KUWALIPA WATU au WAGANGA ili wasiponeshe Mtu waliomroga.


Siku hiyo ikapita Nikalala huku nikiwaza Kesho mchana jua likiwa kali ndio Muda SAHIHI wa Jini kumvaa Zuberi.

Nikawa nacheka meno yangu ya Mbele yote yalioza kwa kula Nyama za Maiti. Nikalala.


ALFAJIRI.


Kwa mtu yoyote yule aliyebahatika kuniona kwa Mara ya kwanza lazima angejua kuwa Mimi ni Mchawi.

Licha ya Kuwa na Nywele ndefu zilikuwa nyeupe km zinajivu, Macho mekundu na ya kutisha, Kucha ndefu lkn pia nilikuwa ninaogopesha tu maana muda mwingi nilipenda kuwa peke yangu.


"Huyu Mtoto anapenda Kukaa chini ya miti mikubwa peke yake halafu utamuona anaongea au anacheka peke yake" yalikuwa maneno ya mama anayeishi katika kijiji chetu akimwambia Mumewe Mara tu walipopishana na Mimi wakielekea Shamba na Mimi nikielekea Shuleni.


Sikuyajali maneno yao kwa sababu nilishayazoea kijijini hapo. Bado Giza lilikuwepo kwani ilikuwa Asubuhi ya saa kumi na moja na nusu.

Siyo kawaida yangu kuwahi Shule Asubuhi na mapema ila kulikuwa na jambo zito la kichawi nilitakiwa kulifanya.


Nilipiga hatua nyingi na kuachana kabisa na yule mama na Mumewe.

Baada ya Kuelekea njia ya Shule nikapita kinjia kinachoelekea makaburini.

Mfuko wangu wa nailoni uliokuwa na madaftari yangu niliushika vyema.

Huku fagio na kidumu cha maji vikiwa mkono wa kulia.


Moja kwa moja nikafika makaburini nilipofika tu nikakuta Wachawi wapatao kumi na Mbili wamesimama wakinisubiri.

Nilipowaona na wao waliponiona walionyesha kufurahi.

Niliwasogelea na kuwa nao sambamba.


"Tumeshukuru Umeitikia wito kwa wakati" alisema Mmoja wa wachawi nafikiri ndio alikuwa msemaji wa msafara wao.


"Tupo hapo tangu usiku wa Jana tukijaribu kuondoka na hii maiti ya Mtoto wa mchungaji lakini Maiti yake haibebeki na haitaki kurudi ndani ya kaburi"

Aliniambia.


Nikasogea zaidi ili kuiona maiti ya huyo mtoto wa mchungaji. Kweli niliikuta imelala juu ya udongo uliofukuliwa kichawi.

Nikasonya kisha nikatamka maneno ya kichawi. Ile Maiti Ikafumbua macho na kunitazama Usoni.


Wale wachawi wenzangu wakashtuka kwa kuona tukio hilo. Nikainyooshea vidole viwili vya mkono wa kushoto kile cha shahada na kile kidogo cha mwisho.

Halafu nikawa nachimba chini kwa kidole gumba cha mguu huku natamka maneno ya kichawi (Sasa hapo nilikuwa naroga na kuwanga juu ya hiyo maiti inisujudie kwa nguvu nilizo nazo)

Ile maiti ikajawa na huzuni na kuinamisha kichwa chini na kuanza kutokwa na machozi.


"Kwanini hutaki kuondolewa Eneo hili?" Niliiuliza Ile Maiti.


"Hapana, sikutaka kubaki hapa kwa uwezo wangu ila kuna nguvu za Mchungaji baba yangu kutoka kwa Mungu ndio zinashindana na nguvu zao za kichawi" alijibu maiti ile.


"Una uhakika baba yako ni mchungaji na ana nguvu za Mungu??" Nilimuuliza.


"Ndio" alinijibu.


"Hapana Baba yako hana nguvu za Mungu pia yeye ni mchawi na anatumia nguvu za kichawi ili ubaki hapa aje na wachawi wenzake wakuchukue wakale nyama yako" Nilimwambia 

Akawa anakataa.


"Hapana Baba yangu hawezi kuwa mchawi" ilisema ile Maiti.


Nikacheka sana.

"Ngoja utaona. Nikauchukua ule ufagio wangu wa shule nikaulaza juu ya Kaburi kisha nikauongelea maneno. 


Pale pale uligeuka na kuwa mfano wa ile maiti.

Nikaongea maneno kaburi la yule Binti (Maiti) likafunguka na nikaiyamuru ile maiti ya pili niliyoibadilisha kutoka kwenye fagio kuwa Maiti ya yule Binti iingie ndani ya lile kaburi.


Ilipoingia lile kaburi likajifunga na kuwa km lilivyoachwa na watu walipomaliza kuzika.


"Sasa utashuhudia Baba yako na kundi la wachawi wakija na kuondoka na mwili ule wakidhani ni wako" niliiambia ile maiti.


Punde si punde wingu likawa jeusi na wachawi wengi akiwemo Mchungaji na Mkewe waliteremka na ungo na kukanyaga ardhi ya makaburini.


Mimi Nilichofanya Nikatamka maneno ya Kichawi na kuyanena Haraka. Pale pale Sisi na ile Maiti ya kweli ya mtoto wa Mchungaji tukageuka kuwa MAKABURI (MATUTA) Kisha tukawa na Uwezo wa kuliona kundi la Mchungaji na WACHAWI wenzie lkn Wao walikuwa hawana Uwezo wa Kutuona.


Mtoto wa Mchungaji hakuamini alichokiona

Alilia na Kuita 

"Baba!Baba!" Lkn Sauti yake haikufika popote na Wala haikuwafikia wale wachawi na Mchungaji.


Kundi Hilo la Wachawi, Walilisogelea Kaburi Kisha wate wakalizunguka Kaburi na kuliweka katikati.

Mkuu wa kundi Hilo akachukua Maji ya Maiti (maji waliooshea Maiti) akawa ana mwagilizia juu ya Kaburi huku akita Jina la Marehem (Mtoto wa Mchungaji)


Kisha Bila Kuchelewa Lile Kaburi likaanza kutikisika na kujigawa katikati

Na ile Maiti iliyokuwa ndani ya Kaburi ilitoka ndani ya Kaburi.

Wachawi wakapiga Makofi na Kushangiria.

Kisha Lile Kaburi likajifunga na kuwa km mwanzo.


Wachawi nao uwa tunavyeo

Basi akaitwa Bi Sauda Yeye kwenye Kikosi Cha Wachawi Ni mtunza Chakula (uwatunza Marehem kwa ajili ya kuwala)

Mkuu wao akamwambia. 


"Kaitunze Nyama yetu Na Usiku wa leo Tutaitafuna na Kumpandisha Cheo SHAYO (Shayo Ni Huyo Mchungaji) 


"Sawa Mkuu" alijibu Bi Sauda. 


Kisha akaichukua Maiti na kupanda nayo Kwenye Ungo.


"Karibia Kuna kucha Sasa Kila mtu arudi Majumbani kuendelea na majukum mengine" alisema Mkuu wao


Kisha kila Mmoja alipanda Ungo wake na kutawanyika. Hapo Mimi Nikatamka Maneno ya Kichawi Tukatoka kwenye Maumbo ya makaburi na kurudi kwenye Maumbo ya kawaida.

Nikamgeukia Mtoto wa Mchungaji. 


"Bila Shaka Umeona na umeamini kuwa Baba yako Ni Mchawi" nilimwambia

Alibaki kimya Hana la Kusema.

Hapo nikawatazama wale wachawi walioniita niwasaidie.


"Kumbukeni wale wachawi wamechukua Fagio na sio Binadamu na tayari amekabidhiwa Bi Sauda, Sasa kabla ya Usiku kufika inabidi Mniletee Mbwa Nyumbani kwetu Kisha Mimi nitajua Nini Cha kufanya" niliwaambia

Wakakubali na kunishukuru Sana.


Mkuu wa Kikosi hiki akamtamzama Mtoto wa Mchungaji na kumwambia

"USIKU wa Leo Tutakukata Ulimi na utajiunga na Misukule wenzako"

Alimwambia, yule Mtoto wa Mchungaji akawa anatia huruma ananitazama Mimi.


Sikutaka Kumtazama Tena, Mimi nikaamua nijigeuze kuwa Paka na Kuondoka hapo Makaburi kwa sababu kazi waliyoniitia nilikwisha ikamilisha.


Bi Sauda alifika Nyumbani Kwake Akiwa na Maiti (Fagio) akapita nayo Hadi Chumbani Kwake na Kuiweka uvunguni mwa kitanda.

Alifurahi Sana.

Kisha akapanda kitandani na Kulala.


SHULENI


Nilifika Karibu na Shule kwa kuwa Ilikuwa bado Asubuh Sana Sikutaka Kuondoka kwenye Umbo Langu la Paka.

Na Muda wachawi Wengi wanakuwa wamesharudi Majumbani kwao.

Shuleni hapo kulikuwa kimya sana, kulikuwa kunaogopesha Sana.

Nilianza Kutembea tembea Kuizunguka Shule.


Mwili wangu ukasisimka Sana na manyoya yakanicheza

Nikajua hapo Kuna Kiumbe au VIUMBE wenye nguvu kuliko Mimi. Ikapidi Nipunguze mwendo na kutembea kwa tahadhari.


Nikasikia harufu ya Pilau na Nyama kwa mara ya kwanza ndio nilikuwa nashuhudia Muujiza wa Majini.

Pilau lilikuwa likipikwa kwa Ustadi na nyama zilizokuwa zinakaangwa.

"Karibu tupike" Sauti iliniambia.


Nilijikuta Natoa Mlio wa Ajabu km vile ukimkanyaga paka Mkia.

Ilikuwa Sauti ya Jini

Uwezo wa Jini Sikuwa nao na Sina nguvu za kupambana nao na walikuwa Majini haswa waliokomaa.


Ndugu Msomaji Kuna Majini wale walioumbwa na Mungu na Kuna Yale Majini ya kutengenezwa na waganga au wachawi (Mdudu) ndio Yale wanayotupiwa watu km Mimi nilivyolitupa uwanjani kwa mama Suma ili limvae Zuberi, kwahivyo ukiwa na jamaa yako au rafiki yako halafu mukajua katupiwa jini basi mutambue huyo wa kutengeneza na ili umtoe ni kumkamata mtengenezaji, maana ndio mwenye nguvu zake.


Sasa hawa Majini walioumbwa na Mungu huwa wanauwezo Mkubwa mno na ndio nilikutana nalo hapo Shuleni.

Nikaanza kutetemeka mwili na kuwa wenye joto, macho yangu yakabadilika mno na kuwa ya njano.

Taratibu Nikashindwa Kuji control nikajikuta narudi katika Umbo la Binadam lkn Nina mkia wa paka.

Na Muda huo Mwanga ulianza kuchomoza na watu walizidi kuamka Majumbani na Wengine walianza kujiandaa kuja Shule.




2--3 mwisho 

🥩😋Utamu wa nyama za watu 😋🥩


Sehemu ya 2


Ilipoishia....... 


Taratibu Nikashindwa Kuji control nikajikuta narudi katika Umbo la Binadam lkn Nina mkia wa paka.

Na Muda huo Mwanga ulianza kuchomoza na watu walizidi kuamka Majumbani na Wengine walianza kujiandaa kuja Shule.


ENDELEA NAYO....... 


Nikakumbuka Jambo la kufanya.

Haraka nikanena lugha ya Kichawi halafu nikanyoosha Vidole vyangu Viwili Kisha nikavikunja na kuvitia mdomoni na kuvipitisha kwenye Koo.

Nikawa nazidi kujipitisha Vidole vyangu kwenye koo (Sio rahis hata wewe Msomaji hapo ulipo ukijaribu kufanya tendo nilalofanya Mimi"

Nilizidi kunena Rohoni lugha ya Kichawi huku nazidi kujisokomeza vidole Rohoni.


Macho yakapanda juu

Nikahisi km Kutapika

Nikazidisha zaidi na nilipozidisha nikaona Muda si mrefu nitatapika.

Na kweli haikuchukua Muda Nilitapika Nilitapika UCHAWI.


UCHAWI ambao unaharufu mbaya ambayo Jini au Majini wakiisikia hawasogei.

Wanakaa mbali na wewe kabisa. Nilipika Sana

Upepo Mkali ukavuma 

Kumbe karibia Eneo zima la Shule kulikuwa na Majini Wengi mno.


Sasa ile harufu ya matapishi ikawa imewatibua walipolala.

Sasa Watu waliokuwa wanapita Karibu na Shule wenye Mashetani wakaanza kupandisha hovyo, maana yale Majini hayakuwa na sehem ya kukimbilia yalizagaa hovyo hovyo Hadi harufu iishe wao ndio warudi.

Palikuwa hapatoshi Uwanja wote wa shule ulitapakaa Majini.


Taratibu ule mkia wa paka ulinywea na nikawa katika Umbo lote la kawaida. Nikakaa tu chini Mana nilichoka.

Baadae kabisa ile harufu ikakata na Hali ikawa sawia ingawa bado baadhi ya Majini walikuwa bado hawajatulia kurudi kwenye sehem zao.


Kengele ya kuwahi Namba ikagongwa, nikatoka Nyuma ya shule nikaenda kupanga mstari wa kuwahi Namba.

Nilipofika nilikuta mistari ya Wasichana na wavulana na Mimi nikapanga ktk mstari wa Wasichana wenzangu.

Nilipotazama niliona Majini nao wamekuja kupanga mstari.

Lakini kwa wanafunz wenzangu hawakuwa wanawaona.


Nilikaa kimya Kisha tukahesabiwa Namba na kuanza kufanya usafi.

Wale Majini nao wakawa wamechanganyika na wanafunzi wanafanya Usafi.

Hali haikuwa nzuri hapo Shuleni. Ikabidi Niende Kumuona mwalimu wa zamu.


"Binti yangu Wande hujambo?" aliniuliza

"Hapana, nimekuja kuomba Ruhusa Naumwa kichwa sijisikii Vizuri" nilimwambia kabla hajanijibu tukasikia Kishindo tukageuka na kutazama na kukuta mwalimu wa Taaluma ameanguka na baiskeli yake na ndio kwanza alikuwa anafika Shule. Akawa anafurukuta na kutupa mikono na miguu km kuku.


Ghafla mwanafunzi mmoja akaanza kupiga kelele km mwenye mapepo. Hapo Roho ikalia paa Nikajua Mimi nimeyatibua Majini Basi siku nzima ya shule wanafunzi na walimu watapata hekaheka Hadi wakome.


Kwakuwa nilishaomba Ruhusa nikaamua niondoke sikutaka Tena Kukaa Kwasababu Nilishajua leo hakutakuwa na masomo Zaid ya dharuba.


Nilipita na kukimbia Kurudi nyumbani Ukiniangalia Ni Binti wa makamo lkn Uwezo wa Kichawi nilionao ulishindana na watu wazima.


Wakati nakimbia kurudi nyumbani Mbele yangu alitokea mchawi mmoja kimuijiza Akiwa amemshika Mmbwa aliyevishwa Sanda.

Nikasimama Kisha Yule mchawi akaniambia.


"Mshirika, Yule mbwa uliyemtaka kwa ajili ya kazi ya Bi Sauda tumekukelea" aliniambia

"Huyu Sio MANUNU?" Nilimuuliza

"MANUNU!!?" alishangaa 

"Ndio, Kuna mbwa amepotea anatafutwa anaitwa MANUNU AU VANILLA" nilimjibu

"Hapana Mshirika huyu tumemnunua" alinijibu

Nilimpokea Kisha Yeye akapotea kimiujiza.


Sasa hapo ikabidi nibadilo njia, badala ya kwenda Nyumbani ilibidi Niende kwa Bi Sauda.

Nilinena maneno ya Kichawi nilipotea ghafla na kutokea nyumbani kwa Bi Sauda.

Nje kabisa ya Nyumba yao nilisimama katikati ya Uwanja Nilimkuta Bi Mdogo (Anaitwa Bi Ashura) mke mwenzie na Bi Sauda akifagia Uwanja wao.


Nilichofanya nikamroga Bila Yeye Kujijua 

Niliiroga nafsi na akili yake ifate kile ambacho Mimi nataka.

Basi Bi Ashura akaja nilipo. 


"Nenda ndani ukaniletee Lile Fagio nililolifanya kuwa Maiti ambalo lipo chini ya uvungu wa Bi Sauda." Nilimwambia

Bila kuchelewa Bi Ashura akaingia ndani haraka Hadi Chumbani kwa Bi Sauda Wakati huo Bi Sauda alikuwa amelala fofofo.


Bi Ashura ikabidi amtoe Yule Maiti, Wao wanaona mait ila Mimi nilikuwa najua lile Ni Fagio Langu la Shule.

Bi Ashura akatoka nae Nje. Nikanena lugha ya Kichawi ile Maiti ilirudi kuwa Fagio Kisha nikamkabidhi Mbwa. 


"Huyu mbwa Sasa nenda kampeleke Chumbani na umuweke uvunguni" nilimwambia

Nae alifanya Bila Kusita 

Mimi nikapotea Kimiujiza na Yeye alipotoka Chumbani akarudiwa na akili yake akaendelea kufagia.


Bi Sauda akazinduka usingizini na alipotazama uvunguni akaona bado Maiti ipo kumbe alikuwa Mbwa, akafurahi Sana.

Akatoka Chumbani na Kukutana na mumewe. 


"Mama Saidi, Nyama Umeiweka Vizuri?" Mumewe alimuuliza. 


Bi Sauda akacheka

"Mmh Mume wangu kwenye chama nimekuingiza mwenyewe mara hii unanifundisha kazi, pita uone Kitoweo kipo kimenona" alijibu Bi Sauda Kisha wote wakacheka.


"Usiku wa leo nitaitafuna Nyama kisawasawa" alisema Mume wa Bi Sauda.


"Haswaaa na ilivyoteke laiiini" alisema Bi Sauda.


Mume akazidi kucheka na kuelekea Chooni

Bi Sauda akatoka nje na Kumkuta Bi Mdogo anamalizia Kufagia.


"Za Asubuh Bi Ashura" 


"Salama tu, Umeamkaje mama Saidi?"


"Mie Namshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kweli Mungu Ni mwema nimeamka salama"


"Eh Jana Msibani ulirudi saa ngapi Mana nilimerudi sijakukuta nikaenda Shamba kuangalia Usalama na wezi" Bi Ashura alimuuliza Bi Sauda.


"Yani Yule Mchungaji amepata pigo kubwa mno analia Sana ,Yani Mungu ampe nguvu kwa kweli. Yule ndie mtoto wake wa pekee" alisema Bi Sauda.


"Mungu atampa subira lakini nasikia eti kafa Kichawi??" Aliuliza Bi Ashura. 


"Wee watu wa Kijiji hiki wana maneno Sana Yani mwenzao kafiwa lakini wanataka wambebeshe fuko la kinyesi aangaike nalo.bHakuna uchawi Wala Lolote.Yule kafa na Corona" alijibu Bi Sauda.


"Eti eh?" 


"Kumbe je, yule Ni Mchungaji mwanae afe kishirikina hata wewe inakuingia Kichwani Bi Ashura?"


"Ndio mana Mimi Nikakuuliza wewe Mkubwa mwenzangu"


"Eeeh awe kaaga hivyo hivyo na ujinga wako, zako sinahesabika" alisema Bi Sauda kwa Mafumbo na kurudi ndani, akaichungulia Tena Maiti akaikuta. akacheka Sana.


Mchana/Nyumbani kwa Mama Zuberi


Lile Jini nililolitupa kwenye maji lilikuwa lipo tayari kumvaa mtoto wa Mwajuma.

Zuberi alitoka Nje baada ya kula Ugari.

Akakatisha katikati ya Sehem nililotupa Jini.

Lile Jini likamvaa Zuberi

Alipiga Kelele Moja tu.


"Mama Nakufaa" pale pale akatokwa haja kubwa na Ndogo, Mdomo ukaenda pembeni mwili wake ukapooza.


Mama Zuberi alitoka ndani mbio 

Alipomuona mwanae chini akaangusha kilio.

"Mamaaaaa weeeeee, Nimekwishaa, wananiulia Mwanangu, Nisaidieni Majirani." Alilia na kupiga makelele


Nikiwa Nipo Nyumbani, nimekaa kibarazani, Taa nyekundu ikawaka kwenye paji Langu la Ishara ya kuwa Jini nililolitupa Limefanya kazi yake.


Haikupita Muda wale wazee Wawili Wachawi wakapita wakitokea Msikitini Nikawaona kwa mbali, Sikuweza kuwafata kwa sababu nilikuwa Nipo Nyumbani, Baba na mama pia Walikuwepo wakianika Mihogo juu ya paa(Makuti) 


Mimi na wale wazee Wawili Wachawi tukatazamana wakatabasam na Mimi nikatabasam

Wakanishukuru Sana. Kisha wakapotea Kichawi.


Nilijua kabisa Zuberi hawezi kupona na Vile nilishamroga mama ake Yani ata wasafiri Dunia nzima bila Mimi Kumuopoa hawezi kupona.


Niliendelea na kazi za nyumbani, kusaidia kutwanga mahindi na Mihogo.

Baba akachukua madumu ya maji na Baiskeli yake na Kuondoka kutafuta Maji.

Mama aliniaga anaenda Kuchukua kuni kwa mama Tedi.


Nikabaki nyumbani peke yangu natwanga Mihogo na mahindi.

Nikakumbuka Mbali Sana, nikakumbuka miaka mitatu iliyopita.

Wakati huo Nilikuwa Mimi na Kaka yangu ambaye Ni Marehem kwa Sasa.


Nilikumbuka kuwa Mama na Baba walikuwa wanatukataza kwenda kwa Bibi na Babu

Walikuwa wakituonya kila siku na tulipowauliza walitujibu tu kuwa mpaka tukiwa wakubwa ndio tutaenda.


Siku moja Mimi na Kaka tukaamua twende kwa Siri kwa BIBI na Babu.

Tulitoroka nyumbani na kwenda. Tulipofika nyumbani kwa BIBI na BABU kwa Furaha yetu tukajisahau kugonga hodi mlango.


Tuliingia moja kwa moja Hadi Chumbani kwao.

Tukawakuta wakiwa Uchi wamelizunguka jiko lilikuwa na Moto na Chungu juu ya jiko walikuwa wanaupika UCHAWI (Wakati huo sikuwa Mchawi na nilikuwa sijui km kuna uchawi wa kupikwa)

Ndani ya Chungu kulikuwa na matunguli, Nywele za Binadam, vichwa vya paka, konokono, viungo vya Binadam na makaratasi meupe yalioandikwa kwa lugha ya kiarabu.


Kulikuwa na Moto lkn vilikuwa haviungui lkn vilikuwa vikipikwa haswa kwa Moto Mkali.

Pembeni yao kulikuwa na SANDA NA MAITI za watu ambao mpaka leo sifahamu Ni kina Nani.


Walipotuona tu walituangalia. Sisi tukabaki Mdomo wazi, Kaka alikuwa na akili kidogo tofauti na Mimi, alishtuka na kukimbia huku analia na Kuita. 


"Mamaaaa, Babaaa,"

Mimi sikukimbia nilisimama tu.


BIBI na Babu wakaniita 

"Njoo Mjukuu wetu eeh njoo ukae hapa" wakiniita na kunishika mkono Kisha wakanivua Nguo zote.


Wakaanza kunilisha Vitu ambavyo sikuwa navijua kwa Wakati ule, wakanichanja na chale mwili mzima na kunipaka Madawa.


Wakanivisha shanga za Kichawi kiunoni, Bibi akatoa Bangili ya mbao yenye Uchawi utosini Kwake kwa kawaida uwezi kuiona hata uwe unamsuka.

Akaiingiza utosini kwangu.

Babu akatoa Chupa ndogo ya kuvunjika mfano wa zile chupa za mafuta ya kunukia Sana.

Aliitoa sehem yake ya haja kubwa Chupa ilikuwa imevishwa Ngozi ya Simba, Chui, mamba, Chatu, Tembo, ilipakwa mafuta ya samaki Papa. Ndani ya chupa kulikuwa na miba mikali ya nungunungu, sindano, na pini.


Wakaichukua Ile chupa na kuniingiza sehem ya uke WANGU.

Baada ya kuingizwa hivyo Vitu Viwili nilijihisi mtu mwenye nguvu na shupavu licha ya umri wangu kuwa Mdogo.


Sikujua kuwa wamenipa nguvu zao zote za Kichawi Tena Uchawi Mkubwa mno na wenye nguvu kama VIUMBE NILIVYOVITAKA hapo juu ambavyo ngozi na mafua yao yamezungushiwa kwenye Kichupa kilichoingizwa kwenye uke WANGU.


Tangu hapo nikawa Tayari nimeshaingizwa kwenye uchawi.

Babu akasogeza Chungu cheusi tiii, lkn kina maji meupe mno.

Kamwagia Uchawi ndani ya Maji halafu akaita


"Koranda! Koranda! Koranda" Kaka akaibuka ghafla kutoka Ndani ya kile Chungu, akiwa amejiinamia Machozi yanamtoka.


Nilifurahi kumuona Kaka sikujua km Bibi na Babu walimuita ili Nimuue.

BIBI akanikabidhi Kisu

"Mchome kifuani, tutakupa Zawadi eeh ya Nyama tamu" alinimbia Bibi.


Nikakipokea kisu na kumchoma Kaka kifuani.

Pale pale akatawanyika na kubaki kisu chenye Damu. Bibi na Babu wakafurahi Sana. Walinivalisha Nguo.


"Nyumbani kwenu ukikuta watu wanalia wewe usilie" waliniambia, nikaitikia kwa kichwa.


Nakumbuka nilirudi nyumbani na kukuta watu Wengi wakilia. Mama alikuwa amepoteza Fahamu halafu baba alionekana km kachanganyikiwa.

Waliponiona walinikimbilia na nikasikia watu wasema. 


"Ameoneka, alipotea kaonekana" 

Sasa sijui walijua nilipotea kiuchawi.

Nilimuuliza Baba Kaka yupo wapi.

Baba alilia Sana na kupiga kifua.


"Kaka yako amefariki ghafla" alisema Baba.

Nilibaki tu kimya namtazama.

Moyo wangu ulijawa na Maumivu mno. Kaka yangu, Ndugu yangu wa Damu aliniuma Sana Moyoni.


Basi hiyo ndio ilikuwa Kumbukumbu ya miaka iliyopita.

Na tangu Nimuue Kaka yangu nilipanda cheo KIJIJINI hapo wachawi Wengi walipata kusikia habari yangu na kuniita Shujaa Mdogo wa Kichawi (Malkia Mdogo wa Kichawi)

Sikutaka kwenda kwa Bibi ingawa mara nyingi nilikuwa nakutana nao huko kwenye Mikutano mikubwa ya Kichawi.


Nilimaliza Kutwanga Mahindi na Mihogo Kisha nikaingiza Vitu vyote ndani Mama akawa amerudi na kuni

Pia Baba nae alikuwa amerudi Kuchukua Maji.


Tukampokea Baba na kuyaweka maji Ndani.

Kisha Mimi na Mama tukaanza kuandaa Chakula Cha jioni.

Wakati huo huo ndio Giza likaanza kutanda na Giza likitanda ndio Utam na Raha ya Wachawi na Mambo kutisha na kuogopesha yanafanyika.


Baada ya Kumaliza Kupika, tuliandaa Chakula na Kula. Tulikula na tulipomaliza Nikatoa Vyombo na Kupeleka Jikoni.


Nikaenda Kuoga na Kisha nikaingia ndani/Chumbani kwangu.

Nikapanda Kitandani na kuutafuta Usingizini.

Huwa nalala halafu Usiku Sana huwa naamka na kukaa Macho tu labda niwe naenda kuwanga au km nina Mkutano na wachawi.


USIKU WA MANANE.


BI SAUDA alimka Kichawi akiwa anatisha Sana.

Akaongea maneno ya Kichawi Kisha akamtoa Yule Mmbwa uvunguni ambaye Yeye anamuona Ni km Maiti ya mtoto wa Mchungaji.


"Nyama yako leo ni Halali yetu" alisema Bi Sauda akimtazama Yule Mmbwa.


Ghafla akatokea Fisi wa Kichawi na kusimama Mbele ya Bi Sauda.

Bi Sauda akacheka. 


"Unaona mkuu amenitumia Usafiri Mkubwa kwa sababu napeleka Nyama. Sitatumia Ungo" alisema Bi Sauda.


Akampandisha Yule Mmbwa juu ya mgongo wa Fisi, Kisha na Yeye akapanda.

Akanena maneno ya Kichawi na bila kuchelewa akawa nje ya Nyumba yao.


Yule Fisi akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka na Kichawi kuelekea kwenye Makutano ya Kundi la Bi Sauda la Wachawi wenzake.


Bi Sauda alitembea Hadi kwenye Daraja refu la kale. Daraja Lililozungushiwa Kamba ngumu, Daraja ambalo lipo katikati ya Msitu.

Chini ya Daraja kulikuwa na maji yanapita lakini hayakuwa mengi

Kando ya hayo maji Kuna mti Mkubwa Sana na wazamani.


Ukipaangalia kwa macho ya kawaida unaweza ukaona kupo kupo tu 

Kumbe wachawi wamejenga mji Mkubwa na wakutisha wenye kubeba Zambi na Maiti za Ajabu.


Kundi kubwa la Wachawi kila siku hukutana hapo na kupeana majukumu na kupanga mikakati yao.

siki (Chachandu ya Mbirimbi) ilikuwa imeandaliwa kwa Ustadi na kuwekwa kwenye machupa yao.

WACHAWI WENGI WANAPENDA PILIPILI ZA MBIRIMBI.

Walikuwa wakicheza ngoma za Kichawi na kufurahi.


Siki ya Mbirimbi iliandaliwa haswaa kwa ajiri ya kulia Nyama ya Mtoto wa Mchungaji.

Na ngoma ilikuwa ikirindima.

WAGENI wa Kichawi kutoka sehem Mbali mbali walialikwa kuja kumpongeza Mchungaji na Kushuhudia akipandishwa cheo kwa kumtoa Nyama Mtoto wake.


Mchawi akitoa nyama Yeye hupewa Ini na ukila Ini Basi utazidi kunogewa kuwaua Ndugu zako kwa Utam wa Ini.

Bi Sauda aliingia Kichwa na kushuka kwenye Fisi

Kila Mchawi alikuwa na hamu ya Kushuhudia Nyama yao inayoletwa na Bi SAUDA.


Walipomuona Bi Saudi walishangaa na ngoma ikazimwa ghafla.

Bi Sauda akashangaa.

Mumewe pia akashangaa.

Wote walishangaa kuona Bi Sauda amekuja na Mmbwa badala ya Mtoto wa Mchungaji.


Mume akawahi kumfata

"Vipi Tena Bi Sauda, Nyama iko wapi?" Alimuuliza. 


Bi Sauda akashangaa

"Kwani Kuna Nyama ngapi !! Zaidi ya hii niliyoileta??" Aliuliza Bi Sauda


"Aiiya!! Huyo sio mtu huyo Ni Mmbwa" Mume alimwambia na hapo kiini macho ndipo kilipo mtoka Bi Sauda na kumtazama Vizuri na kuona amemshika Mbwa. Alishtuka mno na kushangaa. 


Bi Sauda akamuachia mkono Mbwa haraka akapiga magoti.

Mkuu wao akasimama kwa hasira mno na kumsogelea akamshika Yule Mbwa huku anatoa Moshi mweusi machoni ulioenda mwilini mwa Mmbwa, kitendo Cha kumshika tu Yule Mbwa akaanza kupukutika na kuwa Majivu.


Bi Sauda alikuwa anatetemeka.

"Maiti imechukuliwa na Wachawi wengine, Ni WACHAWI gani wanauwezo wa kukushinda Bi Sauda?" Mkuu wao alimuuliza. 


"Hata Mimi nashindwa Kuelewa Hili limewezekana Vipi Mimi kuchukuliwa ile Maiti." Alijibu Bi Sauda.


"Tutaitafuta Ile Maiti na Tutaipata tu lkn ili iwe funzo kwa Watu wa aina yako ambao hamko Makini, WEWE NDIO UTAKUWA NYAMA YETU USIKU WA LEO." Alisema Mkuu na kufanya wachawi wote washangirie.


Mume wa Bi Sauda akapiga Magoti

"Mkuu, Nakubali adhabu uliyotoa kwa Bi Sauda lkn Naomba Umpatie nafasi ya Kuishi ili arekebishe kosa lake. Tuko tayari Kukuletea Nyama Nyingine tofauti na Yeye Wakati tukiendelea Kuitafuta Maiti ya Mtoto wa Mchungaji" alisema Mume wa Bi Sauda.


"Nyama ipi utakayoileta ili Hali Familia nzima umeishaitoa Sadaka?" Mkuu alimuuliza Mume wa Bi Sauda.


"Hapana Mkuu, yupo Mke wangu Mdogo Bi Ashura. Yeye ndiye nitamtoa Sadaka kwa niaba ya Bi Sauda" alisema Mume wa Bi Sauda na kufanya wachawi wote washangirie na kurukaruka.


"Tutawaamini vipi?"


"Naomba utupe nafasi mkuu nakuahid hatutakuangusha"


"Sawa, nakubali muilete hiyo Nyama ya Bi Ashura. Nawapa Siku tatu tu Bi Ashura anatakiwa afe na Nyama yake iletwe hapa hapa tuile Kisha Tukimaliza kumla Nyama Tutapambana kuisaka MAITI ya MTOTO WA MCHUNGAJI NA MCHAWI au Wachawi watakaobainika kutuibia Maiti yetu lazima TUWAKOMESHE NA WAJUTE KWANINI WAMEINGIA ANGA ZETU" Alisema Mkuu wa Wachawi.

Kisha wakaanza Kucheza ngoma. Bi Sauda akawa mpole Hana hata hamu ya Kucheza ngoma.


NYUMBANI KWA MWAJUMA.


Usiku mzima Mwajuma na Ndugu zake hawakulala, walikuwa wanalia tu, Jini nililolitupa Limefanya kazi yake kisawasawa Zuberi alikuwa amekuwa mweusi na kuanza kung'aa km nyoka, miguu ilianza kumvimba.


"Baba Zuberi, mtapoteza mtoto huyu kwanini tusiende kwa Mganga wa hapo kindondo" alisema Dada ake.


"Hapana Dada, Mganga kutoka Bagamoyo Sasa hivi anakuja kasema tusimpeleke popote Yeye Atakuja kumaliza kila kitu" alijibu Baba Zuberi chozi likiwa linamtoka.


"Una uhakika na Huyo Mganga na je kwa Usiku huu atafika kweli?" 


"Ndio Dada, huyo Mganga Ni kiboko anaitwa MZEE PUMBULI NI KIBOKO YA WACHAWI NA MAJINI, Nakwambia Kijiji hiki hatopona Mtu" Alijibu Baba Zuberi.


"Haaiya tumsubiri" Alisema Dada yake kwa shingo Upande.


MAKUTANO YA WACHAWI

MKUU WA WACHAWI akalichota Lile jivu alilopukutika Mbwa Kisha kiuchawi akalisimamisha na kuganda Hewani.

"Wewe jivu la Mbwa nataka Ujiunde na uwe mfano wa Yule alifanya tukio zima la kuiiba Maiti na kukuleta Mbwa, Nataka nimjue Sura yake na km Ni kundi kubwa la Wachawi nataka unionyeshe Sura zao zote mmoja Hadi mwingine" alisema MKUU WA WACHAWI na kuanza Kuroga kwa vitendo na kunena maneno ya Kichawi.

Sasa Lile jivu likaanza Kuutengeza Taswira yangu.


Itaendelea...


#MtotoWaMamaNtilie


🥩😋Utamu wa nyama za watu😋🥩



Sehemu ya 3


Ilipoishia....... 


"Wewe jivu la Mbwa nataka Ujiunde na uwe mfano wa Yule alifanya tukio zima la kuiiba Maiti na kukuleta Mbwa, Nataka nimjue Sura yake na km Ni kundi kubwa la Wachawi nataka unionyeshe Sura zao zote mmoja Hadi mwingine" alisema MKUU WA WACHAWI na kuanza Kuroga kwa vitendo na kunena maneno ya Kichawi.

Sasa Lile jivu likaanza Kuutengeza Taswira yangu.


Endelea nayo..... 


Mganga PUMBULI akaanza kupiga manyanga na kufanya Uganga wake.

Akachukua na kioo kilichozungushwa Shanga Nyeusi, Nyekundu na Nyeupe.

Huku akimmwagia Dawa Zuberi zilizofanana na unga lkn ulikuwa Laini Mno.


Zuberi akaanza kupiga kelele na kuwa na nguvu za Ajabu.

"Mfungeni Kamba, Hilo Ni Jini Lina nguvu" alisema Mganga PUMBULI lakini ghafla nilitokea nikiwa na umbo la Paka.


Nilpojaribu kusogea sehem walipo nilipigwa Shot ya nguvu km ya Radi au Umeme nikatupwa Mbali. Mganga PUMBULI si akaniona akasema kwa Sauti.


"Mwangaaaa huyoooooo" 

Watu wote wakageuka na kunitazama wakaniona lakini waliniona kwenye umbo la Paka.

Nilitazama Vizuri niliona kumezindikwa hivyo nisingeweza kuwasogelea Walipo.


Ikabidi nikimbie, Mganga PUMBULI akanirushia hirizi Nyeusi yenye kamba ile hirizi moja kwa moja ikaja ikajifunga sawa sawa mguuni mwangu (Mfano wa kikuba /kikuku)

Nilihisi kama vyuma vyenye ncha kali vimenitoboa mguuni mwangu.


Mganga PUMBULI akacheka na kusema.

"Kwisha habari yako mwanga Mkubwa"


Niliondoka nikiwa nachechemea.

"Nimempiga pigo la sumu ya Kichawi hatopona katika MAISHA yake, kile Kidonda Cha mguuni kitamtesa na Kumuua" Mganga PUMBULI aliwaambia kina Mwajuma.


"Nataka kumjua mchawi anayenitesea mwanangu" alisema Baba Zuberi huku akiwa na hasira. 


"Muda si mrefu utamjua tu, usiwe na wasi wasi' alisema Mganga Pumbuli....


Nilifika nyumbani nikiwa na Maumivu makubwa mno mguuni.

Nikajibadilisha na kurudi kwenye umbo la Binadam.


Sasa nikakisogelea kile kivuli Cha Mganga Pumbuli. Nikabadilika macho na kuwa ya Rangi ya njano kisha nikakinyooshea Vidole kwa Alama ya Kishetani na Kichawi, nikaongea maneno ya Kichawi huku Moshi ukaanza fukuta kwenye ile hirizi ya Shingoni kwenye kivuli Cha Mganga.

Ikawa inazunguluka zunguka kwenye shingo.


Kule nyumbani kwa Mwajuma, Mganga Pumbuli akaanza kupaliwa na kukohoa, akawa kashika koo lake.


Na Mimi huku nilizidi Kuroga Sasa ile hirizi ikaanza kumkaba kwenye kivuli, na inapo mkaba huku na kule aliyoivaa Shingoni ilianza Kumkaba.


Akashtuka na kuishika, mashale yakamcheza na kuhisi kuwa anarogwa, akataka kuivua lakini haikuvuka.

Akaomba sufuria jeupe pee Kisha liwekwe maji

Wakafanya hivyo na kumpa. Hapo alishahisi kitu kizito Mbele yake.

Akaliweka Chini na kumwagia Dawa ndani ya Maji.


Maji yakazidi kutakata na kuwa meupe pee km Maji ya mto yalio tuama ndani ya misitu. Akajitazama, alijiona yeye lkn hakukiona kivuli chake wala hirizi Shingoni.

Alijiona amekabwa na unjororo wa Moto.


Akaona Basi Mwisho wa Uhai wake umekwisha 

Kitendo Cha kuchukuliwa kivuli sawa na mtu Kuchukua nusu nzima ya Roho yako. Akabaki amepooza tu na kuongea.


"Kijiji chenu nimekivulia Kofia" alisema Mganga Pumbuli.


Mimi nilizidi Kuroga, Mganga Pumbuli akakabwa na ike hirizi kisawasawa, akajishika Shingoni na kupiga kelele, akaanguka chini Kama mzigo, jicho likawa jekundu, shingoni akaanza kukatika katika na Damu zikawa Zina mmwagika.


Familia ya Mwajuma ikabid ikimbie ndani kwa Uwoga, wakamuacha Mganga Pumbuli anapiga makelele huku mwili wa Zuberi ukiwa juu ya kitanda Cha Kamba.

Ile hirizi ilimnyonga ilimnyonga Hadi akakata Roho, shingoni kulikuwa kumetoboka toboka km Chujio.


Alipokufa tu ile Kinga aliyoiweka ikavunjika, na ile hirizi mguuni aliyonifunga ikafunguka.

Na kile kivuli kikapotea na kubaki hirizi.

Nilichukua ile hirizi na kuishika Mkononi na nikaichukua na ile hirizi ya mguuni nikaishika mkononi. 


Hapo Sasa nikawa nina nguvu za Mganga Pumbuli. Nikakusanya mchanga wa eneo la kivuli chake na kufunga kwenye sanda nyeupe ya Maiti ya mtoto.

Kisha vyote nikaingia navyo Ndani.


Usiku huo huo Makundi makubwa ya Kichawi na Waganga wakapata taarifa za kifo Cha Mganga wa Wanganga Mzee Pumbuli.

Wengi hawakuamini hata Kidogo. Nani na uchawi gani ungeweza kumuondoa Mganga Pumbuli ambaye wachawi Wengi wamemshinda.


Mimi nililala lakini mguuni nilikuwa na maumivu makubwa ya kidonda kilichotokana na hirizi ya Mganga Pumbuli.


Nilistushwa na Sauti za watu waliokuwa wananiamsha, nilishtuka na kuamka. Usiku huu na Chumbani kwangu kina Nani waniomshao.


Nilipofumbua macho Vizur sikuamini.

Kwanza Chumba Changu kilikuwa kikubwa kwa miujiza halafu wachawi kibao kutoka vijiji, miji, nchi Mbali mbali walikusanyika Chumbani kwangu Yani walijaa wachawi ambao sikuwaza hata siku moja kama ningeweza kukutana na umati Mkubwa wa Wachawi hao.


Wote walionyesha Furaha mno.

"Hongera sana kwa Kumua Mganga PUMBULI" alisema mmoja wao.

Kwabali nilimuona Bibi na Babu nao wakiwa na Furaha.

Wachawi Wengine kiukweli wanatisha mno, mchawi yeyote anatisha lkn wapo waliozidi kuonekana kutisha.


Wakaanza kunipa zawadi

Zilikuwa Ni Nyama za watu, mapembe, mikia ya sokwe, mifupa ya Binadam, hirizi za Kichawi, Nguo za kuwangia Yani kila Mtu alinipongeza kwa Aina yake.


Waliponiona Mguuni walistushwa na kidonda Changu. Ikabidi kila mchawi atumie nguvu zake Kuroga ili nipone.

UCHAWI upo na utaendelea kuwepo, nilijikuta napona kabisa Tena kwa sekunde chache kutokana na wachawi hao Kuroga kwa kutibu kidonda hiko.


Nikasimama Mbele yao na Kusema

"Asanteni Sana kwa Upendo wenu lakini nichukue nafasi hii kulionya Kundi kubwa la Kichawi la kina Bi Sauda kuachana na Mimi Kwasababu eti niliiba Nyama yao, wapambane na kundi lililonituma kuifanya Ile kazi.

Natoa Onyo iwapo wakigusa anga zangu Nitawaua na Sitaki kulaumiwa" Nilisema kishujaa hata sijajua ni nguvu gani hasa iliyonipa Ujasiri wa kusimama na kutamka maneno mazito.


Kundi la Bi Sauda waliitikia na kukubali kisha mkuu wao akasema.

"Tumegundua kuwa wewe Hauna makosa ila Ni Muda mrefu kundi Lile la Wachawi wa kaskazini Wana ugomvi na sisi wametujaribu na wameshindwa na kwa kuwa leo wapo hapa nataka niwahakikishie VITA YETU IMEPAMBA MOTO, Wafe wao tufe sisi tujajua Mbele. Kitendo Cha kutudhalilisha Mbele ya wageni wetu kutoka Dunia za Kichawi kwa kutuibia Ile Nyama imetuumiza Sana hivyo na sisi hatuja Kubali na Hatuta Kubali LAZIMA Vita iendelee" Alisema Mkuu.


Kundi lake likafurahi na kushangiria. Ghafla ukavuma Upepo mkali wa Ajabu na tukasikia Kishindo kikubwa Sana katikati yetu, Vumbi likatimka, lilitua JINI na kusimama.


Vumbi lilipoisha tukaliona Vizur Lile Jini. (Jini lililotengenezwa na wale wazee Wawili Wachawi, waliouliwa na Mganga PUMBULI)

Lile Jini likapiga kelele kwa hasira.


Mchawi wa zamani Sana (Mwanamke) aliyezeeka akamnyooshea mkono na kuongea lugha ya kijini, Lile Jini likatulia.

Kisha Yule Mzee Mchawi wa zamani Sana akatugeukia.


"Hili Jini tayari limeshamuua Yule Zuberi, kwahiyo Zuberi ameshakufa Usiku huu na hili Jini limetoka mwilini mwa Zuberi na kwenda kwa Wale wazee Ni kama wazazi wake Mana ndio walioliumba lakini alipofika alikuta wamekufa Sasa halijui wapi linaenda, litaishi wapi na litakula nini. Na kuliua halitawezekana na ndio Mana Lina hasira kubwa" alisema Yule Mchawi wa zamani.


"Sasa tufanyaje?" Mmoja wa Wachawi aliuliza.


"Inabidi Tukalitupe Baharini" Alisema Mchawi mwingine.


"Hilo Ni wazo zuri lakini ikumbukwe sehem tulipo na baharini Ni mbali Ni sawa na kutoka hapa kupita Vijiji sita" 


"Haina Shida Tutapaa Usiku huu huu na kwenda kulitupa Baharini"


"Tunalitupaje Sasa"


"Sisi tunaliona Ni JINI HALISI LKN KWA BINADAM WA KAWAIDA ATAMUONA KAMA KOBE WA BAHARINI AU KONOKONO WALE WA BAHARINI" alisema mchawi mwingine.


Basi tukaliamuru Lile Jini liwe ktk Umbo dogo, kisha tukalifunga kwenye Sanda.


Wachawi wote tukaingia kwenye Nyungo zetu, tukapaaa angani.

Safari ya kwenda Baharini ikaanza,

Tuliruka kwa Muda mrefu na hatimaye tukafika Baharini, kilikuwa Kijiji lkn kilichoendelea tofauti na kule tulipo Toka Sisi.


Usiku huo tulikuwa Wachawi Wengi Mno

Ni Wengi kama sisimizi

Tukapanga mstari kwa kuitazama bahari, Yani tulijipanga nusu duara Kuizunguka Bahari.


Lile Jini likatolewa kwenye Sanda na nikapewa Mkononi.

Nikaisogelea Bahari na kugusa maji kwa miguu yangu. Nikaongea maneno ya Kichawi, Upepo Ukavuma, mawimbi yakatawala Baharini. 


Kisha Nikalitupa Lile Jini Ndani ya maji ya Bahari

Likazama na kuibuka Kisha akatutazama sisi Kisha likazama Tena hatukuliona Tena.

Nilihisi Tofauti kabisa Ni kama vile Lile Jini halikupenda Hilo tukio lakini kwa kuwa tulikuwa Wachawi Wengi sikuwa na Shaka.


Tukaambiwa Sasa kila Koo za Kichawi zirudi Vijijini, Mijini na Nchi zilizotokea. Basi tukapanda ungo na kila Mchawi akarudi nyumbani Kwake.


SIKU HIYO ILIPITA

WIKI ILIPITA

MWEZI ULIPITA

MIEZI, MWAKA NA MIAKA ILIPITA.


Nilikuwa Msichana Mkubwa kiasi Mwenye kujielewa.

Sikupata tena kusikia habari ya lile Jini, japo tukio la kulitupa Jini Baharini nilikuwa nalikumbuka vyema.

Niliendelea Kuroga na Kuwanga na Kuua watu.

Hatimaye nilimaliza Darasa la Saba,

Nilifeli, Sikutaka kuolewa na kwa Bahati nzuri nilitafutiwa Kazi za Ndani na Jirani yetu huko MJINI Dar es Salaam.


Nilitaka Kukataa kwa kuhofia kusimama kwa Shuhuli zangu za Kichawi na Uchawi wa kutisha lakini Wachawi wenzangu wakaniambia hata niende Dunia ya wapi Kuroga na kuwanga hakutaisha, ninauwezo wa kuja kila siku kijijini kwetu na Kuwanga.


Hapo nikaamini Sasa naanza ukurasa mpya wa Maisha ya Kichawi huko Dar es Salaam.


Jijini Dar es Salaam.


Usiku Mkubwa Sana Bahari ilikuwa imechafuka mno, mawimbi na Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.

Mawimbi yalipopiga kwa Kasi yakamtoa *KOBE* kutoka Ndani ya Bahari na kumleta Nchi kavu.

Kobe alitembea Hadi kwenye mawe makubwa pembezoni mwa Bahari na kujificha ndani ya Pango.


  Mwisho

Sunday, June 18, 2023

FAIDA YA MMEA WA KIVUMBASI

 

Mti huu wengi huutumia kufukuzia mbu pamoja na

hayo faida zingine ni hizi zifuatazo;-

(1) Hutibu tatizo sugu la nguvu za kiume jinsi ya

kujitibu utachukua kuku jogoo mwenye afya nzuri

mchemshe na majani ya kivumbasi usawa wa fungu

moja la mchicha chemsha katika maji lita 5 tu

utakunywa supu hii siku 4 tu hakika tatizo lako la

nguvu za kiume litatoweka dawa hii ni mujarrabu na

inamajibu yasiyo na madhara kwa mtumiaji.

(2) Huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia

zote unalichemsha hili pamoja na viazi ulaya au vya

chipsi ambavyo havijakaa dukani muda mrefu.

(3) Hufukuza maadui unapoichanganya na udi baada

ya kuikausha na kuisaga unaichoma kama ubani

katika ofisi yako au nyumba yako

(4) Husogeza karibu maruhani au majini wazuri

katika kichwa lugha hii ni ngumu ila wanaojua

wanajua

(5) Kivumbasi pia hufukuza mashetani unakausha

unachanganya na udinadi choma kwa kujifukiza x2

kitwa wiki mbili


na manyoya ya mkiani ya njiwa mweupe mgonjwa

aoshewe na achanganyiwr na mafuta ajipakae

(8) Huondoa migogoro nyumbani unaufikisha katika

maji ya mvua au kisima unamwaga ndani na nje ya

nyumba yako utulivu utapatikana.

(9) huleta bahati karibu hii ni ikiwa hupati kazi


Wahindi wanautumia sana 


Dawa ya uzazi kwa wanawake 


U.T.I,Maralia, taifodi,bawasiri,kisukari,CD 4,n.k

Wednesday, June 14, 2023

TUMIA KITUNGUU MAJI KUJITIBU PID,UTI, KISUKARI, PRESHA NA MAGONJWA MENGINE MENGI KWA DAWA RAHISI INAYOPATIKANA MAZINGIRA YA NYUMBANI KWAKO

 FAHAMU NJINSI KITUNGUU MAJI KINAVYO WEZA KUTIBU UTI N. K

Utumiaji wa kitunguu unaimarisha mifupa ya nyonga

FAIDA ZA KITUNGUU KWA UFUPI
1.Tibu UTI
2.Balance sukari mwilini
3.Mzunguko mzuri wa damu mwilini
4.Kuwa na nywele zenye Afya 
Basi fanya hivi kila asubuhi kabla ya kula chochote 
Katakata kitunguu weka kwenye kikombe Kisha chemsha maji weka kwenye kikombe chenye vitunguu acha yapoe kwa dakika kumi kunywa. 




TIBU MAGONJWA TOFAUTITOFAUTI KWA JIVU LA MAGANDA YA DAFU
Majivu ya magada ya dafu ni dawa nzuri na kwa magonjwa yote ukiamka unahisi unaumwa/kuumwa suluhisho ni Majivu ya maganda ya dafu 

FANYA HIVI KUANDAA DAWA YA MAGANDA YA DAFU INAYOTIBU MAGONJWA KAMA 
1.PID
2.UTI
3.BACTERIA
N.K
Chukua maganda ya dafu choma Pata jivu lake laini weka ndani kwako kila asubuhi kabla ya kula chochote chukua maji ya vuguvugu kwenye kikombe weka kijiko kimoja cha majivu kunywa kila siku utaondokana na magonjwa hatari yote na Utakuwa mwenye afya wakati wote. 

DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU U.T.I


U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.
Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra. Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.
Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.
Kinachosababisha U.T.I:
=>Kisukari
=>Maumivu ya mishipa
=>Ajari katika uti wa mgongo
=>Ushoga (kwa wanaume)
=>Usafi duni
=>Upungufu wa maji mwilini
=>Kushikilia mkojo muda mrefu
=>Kurithi
=>Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.
Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I
=>Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
=>Kukojoa mara kwa mara
=>Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
=>Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
=>Mikojo kukutoka pasipo kutaka
=>Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
=>Kukojoa damu
=>Harufu nzito au mbaya ya mkojo
=>Homa
=>Kusikia baridi
=>Kutokujisikia vizuri
=>Kujisikia uchovu
Dawa mbadala 7 zinazotibu U.T.I
1. Baking Soda
U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi. Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka. Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.
2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):
Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.
3. Nanasi
Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’. Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.
4. Maji ya kunywa
Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji.
Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. Kunywa maji kwa mtindo huu wa jumla, asubuhi kunywa glasi 3, mchana glasi 4 na jioni glasi 3. Glasi 1 = robo lita (ml 250).
5. Vitamini C
Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini
Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo. Vitamini C hukifanya kibofu cha mkojo kubaki na afya kutokana na asidi yake safi kwenye mkojo kitendo ambacho ni mhimu katika kuwazuia bakteria wabaya kufanya makazi kwenye kibofu cha mkojo. Ukiacha machungwa, Vitamini C inapatikana pia kwa wingi katika juisi ya ubuyu na kwenye mlonge. Hakikisha unapata kiasi cha kutosha cha Vitamini C kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na U.T.I.
6. Kitunguu swaumu:
Kitunguu swaumu ni mojawapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bacteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa mhimu katika kutibu U.T.I ya jumla na hata ile ya kibofu cha mkojo. Kwakuwa moja ya kazi ya kitunguu swaumu ni kusafisha mkojo basi ni dhahiri inafaa sana katika kutibu U.T.I. Namna ya kukitumia; Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 10 au 15), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na mapema uamkapo asubuhi kwa siku 7.
7. Limau/ndimu:
Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu. Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na U.T.I na hata kuzuia kutokwa na damu kama matokeo ya maambukizi ya U.T.I hasa kwenye kibofu cha mkojo.
8. Unga wa majani ya Mlonge
Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.
9. Mshubiri (Aloe-Vera):
Chukua jeli ya mshubiri (aloe-vera) vijiko vikubwa vinne, changanya na maji ya kawaida ili kupata kikombe kimoja (ml 250) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 2 au hadi utakapopona. Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.
Katika dawa hizi zote zilizojadiliwa hapa, napendekeza utumie dawa hizi kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kwa haraka, nazo ni; maji ya kunywa, kitunguu swaumu, limau, unga wa majani ya mlonge na mshubiri.
VITU VYA KUFANYA ILI KUJIKINGA USIPATWE NA U.T.I
1. Ongeza unywaji maji kila siku au juisi za matunda, juisi uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.
2. Epuka vinywaji baridi, pombe, chai ya rangi na kahawa.
3. Penda kuwa msafi.
4. Mara zote jitawaze kutoka mbele kurudi nyuma na uepuke kuchangia na wengine vifaa vya bafuni.
5. Pata haja ndogo mara baada ya tendo la ndoa.
6. Usiushikilie mkojo muda mrefu, mara usikiapo kutaka kupata haja ndogo mara moja nenda.
7. Vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kutokana na pamba.
8. Epuka kaffeina.
9. Epuka tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Dawa mbadala hizi 9 zinaweza kukusaidia kujikinga usipatwe na U.T.I au kujitibu ingawa bado inashauriwa kwenda kumuona daktari iwapo maumivu au dalili zinadumu kwa muda mrefu.
       
Lishe: Zifahamu faida 5 kuu za vitunguu 


Kitunguu ni nini? Katika mimea, vitunguu ni sehemu ya familia ya Liliaceae , pamoja vitunguu saumu, na vitunguu maji.    

 Ingawa thamani yake iko chini ya vitunguu saumu, vitunguu vina viungo vyenye ufanisi mkubwa katika kuboredha afya ya mwili. 

Vitunguu huwa sehemu ya vyakula mbali mbali tunavyokula kila siku, vikiwemo vile vinavyoliwa vikiwa vibichi kama vile kachumbari, na saladi, vilivyookwa au kuchemshwa. 

 Kipande cha gramu 80 cha kitunguu (kibichi) huwa na:


Gramu 0.8 za protini
Gramu 6.4 za wanga
Sukari gramu 5.0  
Gramu 1.8 za nyuzinyuzi(fiber)
Miligramu 2.0 za vitamin C.
Kitunguu chenye ukubwa wa kati , chenye gramu 80, ni sawa na kiwango cha milo mitano ya vyakula vyenye kutia nguvu unavyofaa kula kwa siku  

1. Onion ina mchanganyiko wa kemikali zinazozuiakuharibika kwa seli nzuri za mwili   
Vitunguu vimejaa kemikali za mmea, ikiwa ni pamoja na flavonoids, ambazo zote zina uwezo wa kuzuia kuharibika kwa seli na kuzuia majeraha mwilini (anti-inflammatory).

 Vinapoliwa mara kwa mara na katika kiwango kinachofaa, mchanganyiko huu wa kemikali za mme unaweza kukulinda dhidi ya magonjwa ya kudumu kama ile saratani na kisukari.

Ukweli ni kwamba vitunguu huwa vina aina tofauti 25 za virutubisho vya flavonoids na ni miongoni mwa vyakula vyetu vyenye virutubisho vingi.  

 Vitunguu pia vina madini ya salfa. Vimeonyesha kuwa kinga ya aina fulani za saratani 

2. Vitunguu vinaweza kuchangia afya bora
Mojawapo ya viungo vya flavonoids katika vitunguu, quercetin, kina sifa ya kulinda seli za mwili na kuzuia majeraha mwilini. 

 Tafiti zinasema kwamba ulaji wa vitunguu unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa kushusha shinikizo la damu, kudhibiti viwango vya mafuta na kupunguza majeraha mwilini. 

g
Maelezo ya pich,
Vitunguu vimejaa kemikali za mimea, ikiwa ni pamoja na flavonoids, ambazo zinazuia uharibifu wa seli na kuzuia majeraha mwini 

3. Vitunguu vinaweza kusaidia afya ya utumbo   
Kujumuishwa kwa vitunguu katika mlo kuhahusishwa na iuzito wa mifupa. Hii huenda inatokana na kiungo kinacholinda seli za mwili dhidi ya sumu zinazoua seli, jambo ambalo hupunguza uharibifu wa seli na hivyo kupunguza kukonda kwa mifupa.     

 Utafiti uliochunguza athari za vitunguu miongoni mwa wanawake wanaokaribia na waliofikia ukomo wa hedhi unaonyesha kuwa wanawake wanaokula mara kwa mara vitunguu walipunguza hatari ya kuvunjika mifupa ya nyonga. 

 Utafiti mwingine wa wanawake wenye umri wa kati unaonyesha kuwa unywaji wa juice ya vitunguu unapunguza kukonda kwa mifupa na badala yake huongeza uzito wa mifupa. 



Kujumuishwa kwa vitunguu katika mlo kunahusishwa na kuongezeka kwa uzito wa mifupa  

Vitunguu vina kiwango cha hali ya juu cha nyuzinyuzi au fiber, hususan nyuzinyiz ambazo haziwezi kusagwa na tumbo la chakula, ambazo zinahitajika katika kuimarisha afya ya utumbo. 

Ingawa hatuwezi kusaga vyakula vyenye nyuzinyuzi za bakteria , bacteria wanaoishi katika utumbo wetu wanaweza kufanya hivyo na kuzitumia kama petroli ya kuongeza idadi yao na kuzalisha kile kinachoitwa fatty acids (SCFAs).

Tafiti zinaonyesha kuwa SCFA hizi ni muhimu katika kuimarisha afya ya utumbo na hivyo kusaidia mfumo wetu wa usagaji wa chakula na ule wa kinga kufanya kazi vyema.  

5. Vitunguu, hupambana na bakteria 
Tafiti zinaonyesha kuwa vilipotumiwa katika dawa za kikohozi, na mafua , viunguu vilikuwa na viungo vya kupambana na bakteria ...Zaidi ya hayo, ni vitunguu vilivyohifadhiwa kwa muda mrefu vilivyoonekana kuwa na ufanisi zaidi. 

Je vitunguu ni salama kwa kila mtu?
Mzio wa vitunguu ni nadra, lakini baadhi ya watu wanaweza kuupata. Matokeo yake, watu wenye mzio wanaweza kupata matatizo ya usagaji wa chakula, ikiwa ni pamoja na kiunguliwa na gesi tumboni.

 Vitunguu vina FODMAP, aina ya wanga na nyuzinyuzi ambazo mifumo ya usagaji chakula wa baadhi ya watu hauwezi kuzimudu.


Jinsi ya kuchagua na kutunza vitunguu
Vitunguu vinapaswa kuwa visafi na vyenye Ngozi ngumu na laini. Epuka vitunguu vinavyoonyesha dalili ya kuoza.

  

Vitunguu vinapaswa kuhifadhiwa katika chumba chenye joto la kawaida, mbali na mwangaza na katika eneo lenye hewa ya kutosha . Vitunguu vya rangi ya manjano, na nyeundu, vinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko vitunguu maji.

 Vitunguu vyoto vinapaswa kuhifadhiwa tofauti na viazi, kwani vinaweza kufyonza unyevunyevu wa viazi na gesi ya ethylene, inayosababisha viazi kuoza haraka. Usitunze vitunguu katika kifaa au bakuli la chuma, kwani inaweza kuondoa rangi yake.

 Kuhifadhi kwenye friji vitunguu vilivyokatwa kunaweza kuondoa sehemu kubwa ya ladha yake. 

Kiungo cha sulfate, ambacho hutengenezwa wakati seli za kitunguu huzinapokatwa na kupaa ndizo zinazosababisha mtu kutoa machozi.     

 Kupunguzwa kwa uzalishaji wa kiungo hiki, unaweza kupoza kitunguu kwa karibu dakika thelathini kabla ya kukikata.