Wednesday, June 14, 2023

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOANZISHA MRADI WA UZALISHAJI (sana katika ufugaji)

MOMBO YA KUZINGATIA KWA MFUGAJI YOYOTE AU ANAYE PANGA KUWA MFAGAJI BORA BASI MAKALA HII ITAMPA HAMASA KATIKA MRADI WAKE.

                        Mfano wa mradi ufugaji wa kuku 


Miaka ya karibuni kumekuwepo na kampeni kubwa ya maendeleo ya kilimo inayofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa sekta hii kuwahamasisha wakulima kukifanya kilimo chao kama shughuli kamili ya kuwaingizia kipato. Wale ambao walikubali kubadilika na kuzingatia kanuni kwa kuajili watu wenye busara, weledi na maarifa ya usimamiaji wa shughuli hizi hivi sasa wanafaidika nazo, kwani wanapata pesa za kutosha zinazoingia mifukoni mwao kila kukicha na wameweza kuziba mianya yote ambayo hupelekea upotevu wa pesa zao.


Faida kama hizo hazipatikani kwa urahisi. Kuweza kutambua wazo linalofaa kwa biashara pia haitoshi, huu unakuwa ni mwanzo tu. Lazima pesa kwanza ipatikane kama mtaji wa kuendeshea shughuli za biashara husika ili mwisho wa siku zikuingizie ziada ya pesa ulizowekeza (faida) kutokana na mauzo ya biadhaa zilizozalishwa au huduma uliyoitoa kwa wateja. Hapa ndipo suala la kuwa na mipango thabiti ya biashara linapokuja endelea…


NINI MIPANGO YA BIASHARA?

Pale unapoomba mkopo kutoka kwa taasisi husika za kutoa mikopo ambapo mara nyingi huwa ni benki, taasisi zingine za fedha dhahiri kwanza watapenda kujua mpango wako wa biashara (Business plan). Mpango huu utaonyesha malengo ya biashara inayokusudia kuifanya, kwa nini unafi kiri malengo haya yanaweza kufi kiwa, na pia itabainisha mikakati mbalimbali ya kuyafi kia malengo hayo.


Mipango yote ya kuanzisha biashara lazima iwe kwenye nyaraka zilizoandaliwa vilivyo ili kushawishi taasisi za fedha kukuazima fedha.


Bahati mbaya wakulima wengi hawana ufahamu wa kutosha kwenye eneo hili la kupanga biashara za kilimo. Na itabidi ieleweke kwamba bila ya kuwa na nyaraka (documents) itakuwa ni vigumu kumshawishi mtu binafsi au taasisi za kifedha kukuazima fedha zao ili uwekeze kwenye biashara unayotaka kuifanya.


Mpango wa biashara utatofautiana na ukubwa wa biashara, aina za teknolojia zitakazotumika na kwa nani hiyo mipango inakusudiwa. Kwa ujumla mpango wa biashara utatarajiwa kujumuisha vifuatavyo:


• Muhstari wa utendaji mzima (Executive summary): Lengo la sehemu hii ni kutoa picha kamili ya uwekezaji husika. Hujumuisha uanishaji wa biashara yenyewe, mazao au bidhaa, huduma na muhtasari wa uchambuzi wa mikakati ya masoko na mipango ya pesa. Sehemu hii lazima ianishwe kwa upana ili kubainisha mawazo yako na picha kamili ya biashara unayotaka kuifanya. Lazima ubainishe kwa kadiri inavyowezekana dhumuni hasa la pesa unazozitafuta. Na mwisho wa muhtasari huu wa utendaji mzima lazima kuwe na maelezo ya kuvutia ili kumshawishi msomaji wako kwamba biashara hiyo itakuwa na faida. Muda muafaka wa kuandika muhtasari ni baada ya kutayarisha azimio (Proposal) na uingize mwanzoni mwa mpango wako wa biashara.


• Wazo la shughuli husika (Bussness idea): Hii itatoa taarifa kuhusu aina ya bidhaa, zao au huduma utakayouza au kuitoa kwa wateja.


• Mipango ya soko: Hii itajumuisha kila kitu ambacho utakachokifanya kuonyesha nani wateja wako, nini wanahitaji au kukitaka na namna gani ya kuwafi kia. Sehemu hii itatoa maelezo ya bidhaa yako au huduma kwa maelezo ya kina. Pia itajumuisha maelezo ya kiasi cha bei utakayotoza, sehemu ambapo biashara yako itakuwa ikifanyika na njia za usambazaji wa bidhaa au huduma husika utakazotumia na namna ambavyo utainadi (Promote) biashara yako.


• Muundo wa biashara: Hii itaelezea hadhi ya kisheria ya biashara yako, muundo uliochagua kutegemeana na faida na hasara ambazo kila muundo unao. Machaguo ya aina ya umiliki, ubia, au kampuni yenye hisa kikomo au ushirika. Pia katika kifungu hiki itabidi ujumuishe ubainishaji wa namna gani umefi kiria kupitia matakwa ya kisheria na namna ulivyoyatumika katika mchakato mzima wa uanzishwaji.


• Usimamizi: Kifungu hiki kinajibu swali kuhusu aina gani ya ujuzi na weledi wafanyakazi wako wanahitaji kuwa nayo, wangapi utawahitaji na namna ujuzi na weledi wao utakavyosaidia kufi kia malengo ya biashara uliyoyakusudia.


Mipango ya fedha: Utahitaji kuwa na bajeti yakinifu ya biashara yako. Hivyo kifungu hiki itakusaidia kuwa na mipango thabiti kwa faida ya biashara yako na mtiririko mzima wa pesa ya biashara yako hii mpya. Kwa maana pesa inayoingia (mapato) na pesa inayotoka (matumizi). Mara utapokuwa umeandaa bajeti yako utaweza kutumia taarifa hizi kujua kiasi cha pesa utakachohitaji kuanzisha biashara yako. Hii hujulikana kama mtaji wa kuanzia (Start up capital). Itabidi uoneshe chanzo cha mtaji huu wa kuanzia biashara kwa maana ni chanzo kipi kitachangia kiasi hiki na asilimia ngapi ya pesa inayohitajika


DONDOO ZA KUZINGATIA:

• Mtaji: Hii hujulikana kama pesa ya mwanzo ambazo huwekezwa kwenye mradi wa uzalishaji ni vema mkulima akatambua ni chanzo kipi na kwa asilimia ngapi kitachangia kwenye mtaji.


ZINGATIA:

• Mpango wa biashara: Huu ni mwongozo wa kukusaidia kuendesha mradi wako. Hivyo ni vizuri kuwa na mpango unaofaa kukusaidia

kuendesha mradi wako. Huu una msaada mkubwa kwa kuwa ni msingi mmojawapo wa biashara. Kuandaa mpango mzima wa namna ya kuendesha biashara yako hakukuhakikishii mafanikio kwa asilimia mia moja lakini ni njia ya maana kukupunguzia uwezekano wa kuanguka kwa mradi wako. Na ndiyo dira ya uendeshaji wa shughuli zako


JIULIZE:

Kuna maswali muhimu ambayo kila mmoja wetu anapasa kujiuliza kabla ya kuanza miradi ya uzalishaji nayo ni:


• Je, nina muda wa kutosha kusimamia mradi wangu mpya?


• Je, idadi ya kazi zilizopo kwenye mradi husika zinashahabiana na kiasi cha muda nilio nao katika mwaka ambao nitalazimika kufanya kazi?


• Je, mradi wangu mpya utaweza kusaidia utendaji wa shughuli zangu za sasa?


• Je, nina malengo niliyoyaandikisha ambayo yanaelezea matokeo ninayotarajia?


• Je, nina ujuzi na weledi wa kutosha wa kuendesha shughuli za mradi husika?


• Ningependa kusimamia watu iwapo nitahitaji wafanyakazi?


• Nilishawahi kusimamia mradi wowote wa uzalishaji kabla?


• Binafsi Nina nguvu za kutosha za kuendesha mradi?


• Nina ndugu wengine kwenye familia wa kuweza kunisaidia



• Najali kama kuhusu nini majirani zangu wanafi kiri kuhusu mradi wangu?


• Na kwa nini nahitaji kuwa na

mradi huu


MAMBO YA KUZINGATIA KABLA HAUJAANZA KUFUGA KUKU KIBIASHARA ( kuhanzisha mradi)


1. AVAILABILITY (uwepo wako)


Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku kibiashara hakikisha unapata nafasi ya kushiriki kwa karbu katika mradi wako.kama nafasi yako itakua ndogo sana basi jitahidi mwenza wako asimame kama wewe. Au upate kijana mwaminifu sana japo kushiriki mwenyewe moja kwa moja ni bora zaidi .Na ukiona nafasi yako ndogo basi ujitahidi kuhuzuria kwa mda unaoupata usimwamini mtu kwenye ili swala la usimamizi 100%


Watu wengi wameshindwa kuendelea na ufugaji wa kuku kwa makosa ya kutokuwepo karbu na mifugo yake hii inatokana na kumwamini kijana ambaye unampa kazi ya kusimamia mifugo yako anakua makini sana ukiwepo Ila unapotoka na kumwachia Uhuru anafanya Mambo ndivyosivyo.


Umewekeza pesa zako 100% ila uangalizi 10% tuwe serious kidogo.... Uangalizi ukiwa mbovu au muhudumiaji kuku akifanya uzembe kwakua haupo inapelekea kudumaa kwa kuku,Vifo vya Mara kwa Mara ,Uzembe wa kuwapa chanjo,banda kuwa chafu,magonjwa kila kukicha, kupewa report za uongo,kuibiwa kuku ata na mayai yake kwa kuuza n.k so ni muhimu unapotaka kuanza kufuga kibiashara ujitahidi uwe available kwenye eneo lako la ufugaji.


Sijamaanisha kama tusiajiri vijana hapana Ila wengi wao sio waaminifu na ata ukimpata kijana sahihi uwepo wako sehemu ya kufuga ni muhimu sana hii itasaidia kujua hali ya kuku wako kwa kuwaona direct tofauti na mtu anayeendesha shughuli za ufugaji kwa simu


2.COMMITMENT(Kujitoa)


Hakuna mafanikio yoyote hapa duniani ambayo yanakuja kirahisi bila mtu kujitoa na kuchukua maamuuzi magumu...


Ufugaji wa kuku ni kama biashara zingine bila kujitoa uwezi fika popote.. Sikutishi ila nakuambia ukweli hakuna mafanikio bila uvumilivu na subra ata kwenye vitabu vya dini vinatuambia tuwe wenye subra.


Unamtembelea mfugaji unamkuta na kuku broilers wamekua wakubwa wanaelekea kuuzwa ukiwahesabu unagundua ni kuku 1,000 kwa haraka haraka unachukua simu mfukoni au kwenye beg unazidisha idadi ya kuku mara 6,000 bei ya sokoni unapata milioni 6(6,000,000) haraka haraka bila kujua kapitia changamoto zipi mpk kufikia hapo unaenda kununua vifaranga 1,000 chap my friend utakuja kuchukia ufugaji bila kujua makosa ni yako mwenyewe na sio ufugaji...


Unapoanza kufuga jitoe kweli kweli weka imani kuwa hawa kuku ndio ajira yangu,,hawa kuku ndio watanisaidia kuendesha familia yangu,,hawa kuku ndio kila kitu kwangu even if utakua na ajira nyingine aisee ukifanya kazi ya ufugaji kwa kujitoa kama unavyojitoa wakati unafanya kazi za watu amini utashinda


Commitment kupokea changamoto zozote utazokumbana nazo usiwe mtu wa kulaumu laumu sana ila jitahidi kuwa mtatuzi wa changamoto naimani utashinda na ipo siku utakuja kuwa mfugaji mkubwa hapa nchin


3.PASSION (Shauku)


Unapotaka kuanza kufuga make sure unakua na shauku ya kitu unachotaka kufanya.Anza kuwapenda kuku ,penda ufugaji wa kuku,ondoa negativity kutoka kwa watu wanaosema ufugaji mgumu Mara haulipi ww jiandae kuwa na hamu ya kufanya unachopenda


Ukiwa na PASSION utajikuta unakua bize na mradi wako pale unapoanza kwasababu utakua na shauku ya kutaka kuona Jinsi unavyofanikiwa


Watu wengi tumekua na hamasa pale tunapokuwa na mawazo ya kuanza kufuga baada ya kujua faida zake..mwanzo unakua moto sana ila baada ya mradi kuanza unajikuta ile hamasa&shauku uliyokuwa nayo kabla ya kuanza unaiacha.... Sijui unanielewa rafikiii...????


Hamasa ikishuka love ya project inashuka twende kwa mfano:

=unapoanza mradi mwanzoni unakua na passion ya kuwa karibu na mradi wako,mda mwingi unashinda kuwaangalia,ukilala ukiamka unawaza kuku tu but zinapoanza kutokea changamoto let's say za magonjwa,kuku kuanza kufa hapo wengi unakuta anaanza kurudi nyuma bila kujua mda huo kuku ndio wanakuitaji sana kuliko kipindi chochote...

=Baada ya kuku kukua huwajali tena,bandani unaonekana Mara chache unamwachia kijana tu aisee utakuja kushindwa kumbe kosa lako mwanzo ulianza vizuri ila mwishoni ukamalizia vibaya


Tuwe na PASSION ya mifugo yetu pale tunapotaka kuanza na baada ya kuanza..


4.LOCATION (sehemu ya kufugia)



Muhimu unapotaka kuanza kufuga angalia sehemu unayotaka kufuga unaweza jiuliza maswali yafuatayo:-

=Je..?? Vip kuhusu huduma ya barabara,maji na umeme..

=Je wafugaji walionizunguka wanafuga zaidi kuku aina gani km wanafuga broilers mm ngoja nifuge layers niuze mayai

,,,wafugaji walionizunguka wanafuga zaidi chotara mm ngoja nifuge kienyeji

,,,,maeneo niliyopo watu wanafuga sana kuku wa mayai mm ngoja nifuge chotara kwaajili ya kuuza kuku wa nyama n.k

Ni vyema kujua location uliyopo na market ya hiyo sehemu hii itakuepusha kufuga kuku ambao ukija kwenye soko unapata shida kuuza kwa wakati inaweza ikakurudisha nyuma na kukataa tamaa...


Hakikisha location yako inakua rafiki na ufugaji wako jenga banda sehemu nzuri kuepuka changamoto zisizo za lazma


5.RESOURCES (Rasilimali)


Waoo tunamalizia sehemu ya 5 baada ya hapa waiting kwa somo jipya

RESOURCES unapotaka kuanza kufuga hakikisha unajiandaa ata km kipato chako kidogo basi jiandae kutokana na level ya kipato chako,,,,


Maana yangu ni ipi unapotaka kuanza kufuga gharama za ufugaji zipo wazi kabsa.


1.Ujenzi wa banda pamoja na vifaa vyote kwa ujumla mf vyombo vya chakula na maji n.k

2.chakula cha kuku

3.kuku wenyewe

4.Chanjo mbalimbali

Sasa unakuta mtu anaanza kufuga kisa tu kajenga banda hapa banda peke yake alitoshi kuwa mfugaji


Mfano kuku aina ya layers yaan kuku wa mayai wao ukianza kufuga inachukua almost miezi 5 mpk 6 kuanza kutaga kwahyo kwa kipindi hiki chote hakuna utakachokuwa unakiingiza zaidi ya pesa kutoka tu Je...??? Umejiandaa vipi na kulisha kuku miezi yote hyoo????


Kwahyo unapotaka kuanza kufuga jiandae na vitu muhimu km kuandaa chakula ili unapoanza kufuga iwe rahisi kwako,,, unaweza nunua mazao kipindi cha mavuno kwa bei rafiki ukaweka store... Sio lazma kununua chakula cha dukani unaweza nunua nafaka kutoka kwa wakulima na ukatengeneza chakula chako cha mifugo kwa bei cheee


Angalia mfuko wako na anza kufuga kutokana na kipato chako

Mfano unaweza kuanza na broilers ambao utawalea ndani ya week 4 wanakua tayari kuingia sokoni ukafanya hivi ili kukuza mtaji wako,,, ukiona hii uwezi bhasi unaweza ukaanza kufuga kuku wa kienyeji kwa kununua rika ambalo tayari limeanza kutaga ili usitumie nguvu kubwa sana ni kitendo cha kuwa chukua na kuanza kufuga baada ya mda mfupi wanataga na kuanza kutamia,, final km upo vizuri unaweza anza na kuku wa mayai au ata chotara ukafuga


Muhimu anza kufuga kutokana na uwezo wako usiforce kufanya vitu oversize utakuja kufail mchana kweupe...


NAMNA YA KUANZISHA MRADI


i>>Ukishapata mtaji tulia na omba ushauri kwa wazoefu juu ya mradi wako-uwe makini na watu utakaowaomba ushauri.


ii>>Fanya utafiti wa kutosha kuhusu mradi wako,mfano utafiti wa masoko,usifanye mradi kwa kuiga (kufuata mkumbo)


iii>>Fanya mradi ambao unaupenda

iv>>Fanya mradi ambao una ujuzi nao kama hauna ujuzi nao unaweza kuanza kwa kiasi kidogo


v>>Hudhuria semina za kimaendeleo au soma vitabu vya kukufanya uelewe namna ya kuendeleza mradi huo.


vi>>Fanya biashara halali na kama kubwa kidogo inahitaji leseni basi itafute leseni husika.


MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUBORESHA MRADI WAKO


1>>Tafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza mradi wako


2>>Usikate tamaa kwa changamoto/misukosuko unayoweza kukutana nayo njiani.


3>>Ufanye mradi wako na mambo yote kwa bidii kubwa


4>>Jiwekee malengo ya wiki,mwezi na mwaka


5>>Uwe mbunifu na unayekubali kujifunza mambo mapya na kukubali kubadilika


KUMBUKA 

Soko ni kitu cha muhimu katika mradi wako kwa sababu mwishoni ukishapata mavuno yako kwa shughuli za itahitaji uziuze hivyo kuwa makini na mradi unaochagua kwa sasa miradi ambayo soko lake ni rahisi kulipata ni Kuku wa kienyeji, kuku wa mayai/nyama matunda,mbaazi,ufuta n,k

 

  JE WAJUA 

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓

Umuhimu Wa Kuweka Viota Vya Kutagia Ndani Ya Banda Lako...


Kiota Ni Sehemu Ambayo Kuku Anaitumia Kwaajili Ya Kutaga Mayai Yake Japo Wengi Wetu Hatujui Umuhimu Wa Kuweka Viota Na Kupelekea Kupata Hasara Ya Kupoteza Mayai Bila Kujua Au Kwakujua Ila Tunadharau...


Unatakiwa Kujenga Viota Mapema Ili Kuku Azoee Mapema Kabla Hajaanza Kutaga Ni Tofauti Na Watu Wengi Ukumbuka Kutengeneza Viota Baada Ya Kuku Kuanza Kutaga Na Kupelekea Changamoto Ya Kuku Kutaga Sehemu Yoyote...


Madhara Ya Kutokuweka Viota Ni Kama Ifuatavyo...


1️⃣Upotevu Wa Mayai


2️⃣Kuku Kutaga Sehemu Yoyote Na Kupelekea Ugumu Wa Kukusanya Mayai


3️⃣Inasababisha Kuku Kudonoa Mayai Yao


4️⃣Inapelekea Mayai Mengi Kuvunjika Kwa Kukanywagwa


5️⃣Usalama Wa Mayai Unakua Mdogo Sana


🪹🪺🪹Kutoka Na Hizo Changamoto Anazoweza Kupata Mfugaji Ni Muhimu Kutengeneza Viota Mapema Ili Kuepusha Hizo Changamoto...


Sifa Za Kiota Cha Kutagia Inatakiwa Iwe Kama Ifuatavyo...


1️⃣Kiota Kinatakiwa Kiwe Kikubwa Na Chenye Nafasi Ya Kutosha Kumruhusu Kuku Kutaga Vizuri...


2️⃣Kiota Kinatakiwa Kiwe Sehemu Yenye Utulivu Yaani Kuku Akiingia Asipate Usumbufu Wowote...


3️⃣Viota Vinatakiwa Viwe Vingi Kulingana Na Idadi Ya Kuku Ili Kuepuka Usumbufu Wa Kuku Kung'aniana Sehemu Moja Wakati Wa Kutaga...


4️⃣Kiota Kinatakiwa Kiwe Safi Mda Wote Ili Kuepusha Wadudu Wasumbufu Kama Vile Utitiri 🪳 Viroboto 🐞 Mbu 🦟 Sisimizi 🐜 N.K...


5️⃣Kiota Kinatakiwa Kiwe Na Maranda Au Nguo Ili Kuzuia Yai Kujigonga Wakati Wa Kutagwa Au Unaweza Tengeneza Mbao Raini Itakayoruhusu Kuku Kutaga Bila Kuvunja Yai Lake...


6️⃣Kiota Kinatakiwa Kisiwe Wazi Sana Yaani Kinatakiwa Kiwe Na Giza Fulani Hivi Hapo Kuku Ndio Anajihisi Huru Zaidi Na Pia Inapunguza Kuku Kudonoa Mayai Yao Tofauti Na Kiota Ambacho Kinamwanga Mkali Ni Rahisi Kuku Kushawishika Kudonoa Mayai Yao...


7️⃣Kiota Kinatakiwa Kisiwe Sehemu Ya Juu Sana Kiasi Kwamba Kuku Anapata Shida Kukifikia Tengeneza Mazingira Rafiki Ili Kuku Asipate Usumbufu Anapotaka Kutaga...


NB: Tujitahidi Kuweka Viota Mapema Kabla Kuku Hawajaanza Kutaga Ili Kuepuka Usumbufu Wa Kuweka Baada Ya Kuanza Kutaga Halafu Kuku Wakawa Wanataga Nje Ya Viota...



Ujifunze Mambo Mbalimbali Kuhusu Ufugaji Wa Kuku...

 KUKU WA ASILI AKAE PEKE YAKE BILA KUCHANGANYWA NA MAKUNDI MENGINE YA NDEGE WAFUGWAO.



Muhimu kuamua kundi lipi utahusika nalo kwenye ufugaji kabla ya kuingia hasara kubwa.


Kumekuwepo na shida kubwa kwa wafugaji kuchanganya mifugo mingi kwa wakati mmoja.


Sio ajabu ukakuta mfugaji ndani ya banda moja ameweka bata, kuku, kanga, njiwa n.k


Yaani inakuwa haifahamiki kama hilo ni banda la kuku au ni mfugo upi hasa anakusudia kuupatia kipaumbele.


Na shida hii inatokana na kwamba wafugaji hao, wanafuga bila malengo na bila kujipanga wapi wanapotaka wafikie kibiashara.


Mbali na kwamba unapochanganya makundi tofauti ya ndege unawahatarisha kiafya hasa ukizingatia wengine wanashambuliwa magonjwa mapema na wengine wanahimili magonjwa, ila pia unatumia gharama kubwa pasipokuwa na manufaa halisi ya gharama hizo.


Pia ufugaji wa namna hii unapelekea vifo vingi vitokee kwenye mifugo yako kwa kuwa wanaambukizana magonjwa kwa njia tofauti, na kuna uwezekano wa kuzalisha mlipuko wa ugonjwa mpya eneo hilo.


Mfano, bata ana asili ya uchafu kuanzia kinyesi chake na hata kupenda kuishi kwenye maji machafu.


Mazingira kama hayo kwa kuku ni hatari kwani yanamsababishia magonjwa kama typhoid, minyoo, kuhara n.k


Ukiona unawachanganya kuku na ndege wengine, basi ujue utaendelea kupata hasara kutokana na milipuko ya magonjwa na vifo.


Kama unataka kuwa na mifugo yote kwa wakati mmoja, basi ijengee miundombinu yake kwa kila kundi na uwatenganishe bila kuwaweka sehemu ya karibu.


Ukifuga kwa kufuatisha utaratibu sahihi, kuku wa asili wanauwezo wa kuongezeka haraka na kukupatia matokeo chanya 

   ZINGATIA!! 

NAKUSIHI MFUGAJI KUTEMBEA MAKALA HII MARA KWA MARA KUNA MASOMO MAZURI YA TOKA KILA SIKU KUHUSU UFUGAJI WA KUKU. 

T + F + A = A Mawazo husababisha hisia. hisia husababisha hatua. na hatua husababisha matokeo

0 comments: