Thursday, June 1, 2023

SODA INAMARA MAKUBWA KULIKO SIGARA(mvutaji wa sigara ni bora kuliko yule anaye kunywa soda kama kinywaji pendwa kwake bila kujua anajua huku akijiona makala hii imesheni madhara makubwa ya soda kwa binadamu inatisha mno)

KUMBE MVUTA SIGARA NI BORA KULIKO ANAE
KUNYWA SODA KILA SIKU KAMA MAJI KWAKE. 



Unaependa kunywa soda?
Soma hadi mwisho 
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi
wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative
Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na
tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika
afya ya umma duniani,umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari
kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya 
kansa katika mwili wa binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa
yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda
yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza
na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake,
bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.
Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni
ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa
maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara
makubwa katika mwili wa binadamu.
 
                   
Utafiti wa lIJUTA unaonyesha kuwa utamu wa
kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomondani
ya soda.
IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilichobadili ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwsababu
ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia
kinywaji hicho.
Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya
soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji
kuwa teja wa kinywaji hicho.
                   


Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa
soda huwekewa 'fructose' (sukari) nyingi kupitia
mfumo wa sirapu
ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa
ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa
mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi
sasa na dunia kwa ujumla.
Marekani imeshapiga marufuku matumizi ya soda
kwa watoto wenye umri chini ya miaka 12.


Dk. Mercola, mtaalamu wa masuala ya lishe asilia
na tiba Marekani, amekaririwa akieleza kuwa soda ni
hatari kwa binadamu
sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi.
Watumiaji soda wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa
cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya
kupidukia na asidi kali ambayo huvuruga afya zao
sana.

soda imepigwa marufuku kutumiwa na watoto walio
na umri chini ya miaka 12 na walio shuleni katika
baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani, kutokana
na madhara ya kiafya yanayosababishwa na kinywaji
hicho.
Huku bongo,soda ndio kinywaji cha watoto na
wangonjwa daaha ni hatari sana.

            


Soda haina lishe ya aina yoyote
zaidi ya maji na sukari.
unywaji wa soda huongeza kiasi
kikubwa cha madini joto.

Madhara ya soda ni makubwa
kuliko ya uvutaji sigara.
Ukiweza acha au punguza kunywa
soda.
Usiwape watoto soda,wafundishe
kunywa juice za matunda asili.
  



N.B
Kunywa maji au juice ya matunda asilia ni bora kuliko unywaji wa soda. Kuwa na nidhamu juu ya Afya yako leo ili ufurahie ukuu wa muumba wetu uwapo duniani 

Penda sana kutumia chakula kama dawa na sio dawa kama chakula. 
Siku zote chakula ni dawa kuwa ni mwenye nidhamu kwa kile unacho weka kinywani mwako kama hakina faida yoyote kwenye mwili niheri ukaachana nacho kabisa. 


T + F + A = A Mawazo husababisha hisia. hisia husababisha hatua. na hatua husababisha matokeo

0 comments: