Sunday, May 28, 2023

BIASHARA NDIO MAISHA HALISI , KOSA 1 KUBWA LINALO WA GHARIMU WA FANYA BIASHARA WADOGO(wenda hata wewe lina kugharim twende pamoja kwenye makala hii๐Ÿ‘‡)

 BIASHARA NDIO MAISHA HALISI



Kwa kuangalia hili haraka haraka, duniani hapa ukitaka kutimiza ndoto zako basi huna budi kufanya biashara.


Biashara ni kitendo Cha kununua bidhaa na kuuza bidhaa Kwa lengo la kupata faida au pesa ya zaidi.


Biashara ni kitendo Cha kuuza thamani uliyonayo ili kupata fedha yaani value for money.


Kwa tafsiri hizo chache japo zipo tafsiri nyingi kuhusu biashara lakini Leo ni-generalize kwamba biashara ni๐Ÿ‘‡


 kitendo Cha kununua na kuuza bidhaa, ni kitendo Cha kuzalisha na kuuza bidhaa, ni kitendo Cha kutoa huduma Kwa lengo la kupata faida au fedha ya ziada , ni kitendo Cha kuuza kipaji ulichonacho, maarifa uliyonayo, ujuzi uliyonao, elimu uliyonayo au chochote kitu unachokijua katika maisha au unachokifanya ili kupata fedha au Kwa lengo la kupata fedha.



Sasa Kwa nature ya ulimwengu huu ukitazama Kila kitu ni biashara mfano kazi za serikali ni biashara ya serikali, kazi za kilimo ni biashara ya kilimo, kazi za elimu ( mashule, vyuo n.k) ni biashara za elimu, kazi za hospital, udaktari ni biashara za kutoa huduma za kitabibu, zipo biashara nyingi sana ambapo nikianza kuziorodhesha hapa sintomaliza Leo Wala kesho.



Kwa mantik hiyo utaona kwamba maisha ni biashara, ili uweze kuishi na kufanikisha ndoto zako huna budi kufanya biashara ya kile unachokijua, ya kile unachokifanya namaanisha kibadilishe kiwe biashara , hayo ndio maisha halisi ya kutimiza ndoto zako otherwise utakuwa unatimiza ndoto za wengine waliyoamua kubadili kile wanachokifanya , wanachokijua kuwa biashara hivyo watakupa ajira Kisha watakulipa mshahara yaani posho.


naposema posho namaanisha kwamba mtu anatumia muda wako, nguvu zako, elimu Yako, ujuzi wako na maarifa Yako kufanya biashara yake ( kazi katika kampuni au serikali au wherever ) na Kwa kupitia kutumia nguvu zako hizo, akili zako, uwezo wako unamzalishia faida ya million kumi Kwa mfano Kwa week mbili au million 20 Kwa mwezi Kisha yeye anakulipa laki 7 au 8 kama mshahara ( hiyo inaitwa posho maana ulichokizalisha hakiwiani na unachopewa hata robo ).


Hivyo bas ukishindwa kuwekeza mawazo Yako, akili Yako, uwezo wako katika kujiajiri kwenye biashara au ukishindwa kubadili kile unachokijua katika maisha au kile unachokifanya katika maisha kiwe biashara na Kisha kufukuzia ndoto zako kupitia mabadiliko hayo basi Kuna ambao watajiajiri katika biashara, watabadili kile wanachokijua katika maisha, watabadili Ile elimu Yao au kile wanachokifanya kuwa biashara na badae watakuajiri wewe na kutimiza ndoto zao.



Biashara ni simple tu Kwa kuwa siku zote ukitaka kufanya biashara, angalia eneo lako ulilopo, unaloishi ni kitu Gani kinawasumbua, ni changamoto Gani inawakumba, ni matatizo Gani yanawasumbua , ni bidhaa Gani haipatikani eneo Hilo na watu wa hapo wanaihitaji Kwa wingi na wanaipata Kwa shida.. 


ukishajua na kugundua hivyo tafuta majibu ya hayo matatizo, ya hizo changamoto au hiyo bidhaa inayopatikana Kwa shida na inahitajika sana then hayo majibu wauzie na hiyo ndio biashara na utatoboa , utafanikiwa moja Kwa moja pasipo kipingamizi.


Biashara ndio chimbuko la utajiri, hakuna namna unayoweza kuwa tajiri kama hufanyi biashara Tena Kwa kufuata kanuni zote za biashara, kujua elimu ya fedha na uwekezaji pamoja na budget.


Nionyeshe tajiri asiyekuwa mfanyabiashara jibu ni hakuna tajiri ambaye siyo mfanyabiashara


swali ni je Kwa Nini wewe hutaki kufanya biashara?? na unataka kuwa tajiri, kuwa na maisha mazuri, kuwa na fedha nyingi, kuwa na uhuru binafsi katika maisha, kuwa na uhuru wa kifedha.


Huwezi kupata vyote hivyo kama hufanyi biashara,utaishia kuajiriwa( kufanya biashara za wengine) utaendeshwa kama gari mbovu, utashinikizwa kama compressor mbovu, utagombezwa , utatumiwa full time na Kisha kulipwa posho na usipojiongeza unakufa maskini kabsa au mtu wa kipato Cha kawaida sana yaani mediocre.



Biashara ni akili tu, Haina haja ya kuwa na mtaji fedha Tena siku hizi unafanya affiliate marketing unapata mtaji at the same time unajifunza biashara ukishaijua na mtaji umeupata katka kufanya hiyo affiliate marketing ukianza biashara Yako utaifanya Kwa usahihi sana maana tayari


๐Ÿ›‘ *Kosa 1 Kubwa Linalowagharim Wafanya Biashara Wadogo. ( Huenda Na Wewe Linakugharim )*


Mafanikio Katika biashara yana siri nyingi sana ambazo wewe kama mfanya biashara,


Ni muhim sana kuzijua siri hizo, hata kama sio Zote.


Vinginevyo unaweza kujikuta unafanya biashara kwa muda mrefu sana,


Pasina kuwepo na mabadiliko yoyote yale katika biashara yako,


Na hii ndio sababu ni muhimu kwa mfanyabiashara kuwa na nidhamu ya kujisomea pamoja na kuongeza ujuzi kila siku,


Ili kuweza kuzifahamu siri hizo hata kama sio Zote.


Baada ya hayo, leo nilitaka nikukumbushe kunako kosa 1 ,


Linalo tugharim wafanya biashara wengi wadogo,


Na hivyo limepelekea biashara nyingi ndogo kuendelea kuwa vile vile,


Na biashara kubwa kuendelea kunawiri na kung'aa.


Kosa lenyewe ni kutokuwa na PLAN Katika biashara yako,


Plan kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni mpango mkakati katika biashara Yako.


Plan katika biasharaa ni kitu muhim sana haijalishi ni biashara kubwa au ndogo.


Kwa sababu plan ( mpango mkakati wa biashara)


Ndio utakusaidia kukupa uelekeo ( direction ) Katika biashara Yako,


Plan ndio itakuonesha nini ufanye katika biashara yako,


Ili biashara yako iweze kupiga hatua moja kwenda hatua nyingine.


Lakini cha kuskitisha zaidi ni kwamba wafanyabiashara wadogo,


Wengi wetu, huwa tunajisahau sana katika msingi huu.


Utakuta Mfanya biashara, anafanya biashara lakini ukimuuliza,


Ni kiasi gani cha pesa unakusudia kuingiza mwezi huu katika biashara yako??


Wengi utakuta hawajui kabisa, wao wanafanya tu bora liende,


Mwingine utakuta kapanga kiasi, lakini ukimuuliza,


Ni nini unakusudia kufanya ili kupata hicho kiasi ulicho kusudia??,


Utakuta hajui, yeye alicho nacho ni matamanio tu.


Je una plan yoyote ya kuongeza ujuzi utakao kusaidia kuikuza biashara yako??


Je unaiona wapi biashara yako baada ya miaka mitano???


Je plan yako katika uwekezaji ni ipi?? Uwekezaji katika matangazo, bidhaa n.k


Wengi katika wafanya biashara wadogo utakuta hawana kabisa majibu ya maswali haya,


Naomba na wewe usiwe miongoni mwao.


Mtu mmoja aliwahi kufeli kupanga ni kupanga kufeli ( Fail to plan, plan to Fail )


Usikubali kabisa kuendesha biashara bila kuwa na uelekeo wowote ule,


Hata kama ni biashara ndogo Kiasi gani, hakikisha unakua na mpango wa ukuaji katika biashara Yako,


Usifurahi tu kuishia kupata hela ya kula na kulipa kodi,


Lengo la biashara sio hilo, lengo la biashara ni siku moja ufikie level ya uhuru wa kifedha,


Level ambayo utakuwa na uwezo wa kuingiza pesa hata ukiwa umesinzia. 


Kumbuka,


Kuendesha biashara bila kuwa na mpango wa ukuaji 


Ni sawa na captain anae endesha meli au au rubani anae endesha ndege bila dira ya uelekeo wa anako kwenda.


Ni ngum kufika na hata akifika atafika amechelewa sana.


Plan, Plan , Plan.


It's me,


@Content creator 

T + F + A = A Mawazo husababisha hisia. hisia husababisha hatua. na hatua husababisha matokeo

0 comments: